SUMATRA MBEYA YABATILISHA MGOMO WA WAMILIKI WA DALADALA.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sumatra-mbeya-yabatilisha-mgomo-wa.html
Mamlaka ya
usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra) mkoani mbeya imelaani mgomo wa
wamiliki wa mabasi madogo ya abiria maarufu kwa jina la daladala ambayo
yanafanya safari zake kati ya stendi kuu na uyole jijini mbeya kwa madai
kuwa mgomo huo ni batiri huku ikiwaagiza wale ambao hawajarejesha
magari yao barabarani kuanza kutoa huduma ya usafiri mara moja kabla
mamlaka hiyo haijachukua hatua ya kufuta leseni zao.
Meneja
wa sumatra mkoani mbeya ndiye ambaye ametoa tamko hilo ambapo amesema
kuwa madai ya madereva wa mabasi hayo kuwa njia mpya ambazo zimeanzishwa
na sumatra ni ndefu hayana msingi wowote kwa vile umbali uliopo
haujazidi kiwango cha nauli kinachotozwa kisheria huku akiwataka
madereva kurejesha huduma zao mara moja kabla hatua ya kufuta leseni zao
hazijachukuliwa.
Katika
hatua nyingine, Chacha amewaonya madereva na makondakta wenye nia ovu
ya kuzuia wenzao wenye nia njema ya kutoa huduma, kuwa waache tabia hiyo
kwa kuwa wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Kaimu
mkurugenzi wa jiji la mbeya, Dk. Samwel Razaro amesema kuwa mgomo wa
madereva wa mabasi hayo imeleta athari kubwa kwa wakazi wa jiji la mbeya
na halmashauri, kutokana na mapato ya jiji kushindwa kukusanya mapato.
Kwa
upande wake, mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala wa jia kuu ya
uyole, sande mwakyusa, amesema kuwa baada ya kusikiliza uamuzi wa
serikali anapeleka ujumbe huo kwa madereva wenzake ili waamue hatua
zaidi za kuchukua.
