SIMBA WASIOFUGIKA WAPAKATWA NA CROATIA...EKOTTO AZUA TIMBWILI NA MWENZAKE, AMPA CHA MOTO..
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/simba-wasiofugika-wapakatwa-na.html
HASIRA za Benoit
Assou-Ekotto ziliishia kwa mchezaji mwenzake Benjamin Moukandjo baada
ya kuamua kumpiga kichwa katika dakika za mwisho za mechi hiyo.
Cameroon waliloweshwa 4-0 na Croatia
katika dakika za majeruhi na beki wa kushoto wa Tottenham ambaye alikuwa
anacheza kwa kwa mkopo QPR msimu uliopita aliamua kumshambulia mchezaji
mwenzake.
Assou-Ekotto alishikwa na hasira baada
ya kipyenga cha mwisho kupulizwa mjini Manaus na Samuel Eto`o
alilazimika kumtuliza ili arejee katika hali yake ya kawaida.
Tulia mwanangu, wewe ni proo!: Mshambuliaji wa Cameroon , Samuel Eto'o akimtuliza Assou-Ekotto baada ya kipyenga cha mwisho.