SIMBA SC YAWAALIKA WANACHAMA, WANAHABARI KUONA MAENDELEO YA UWANJA BUNJU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/simba-sc-yawaalika-wanachama-wanahabari.html

AZAM
FC pekee ndio klabu ya Tanzania yenye uwanja wake wa kisasa kwa ajili ya
mazoezi, mechi za ligi kuu na michuano yote inayosimamiwa na shirikisho la soka
barani Afrika, CAF.
Katika
historia ya soka la Tanzania, Azam fc haiwezi kunusa ukongwe wa klabu mbili za
Simba na Yanga.
Hizi
ni klabu zenye mafanikio ndani na nje ya uwanja. Ni klabu zenye mashabiki kila
kona ya nchi hii.
Lakini
licha ya kukaa miaka mingi katika soka la ushindani nchini Tanzania na michuano
ya Kimataifa, Yanga na Simba hazijawahi kumiliki viwanja vyake vya mazoezi na
mechi za ligi kuu.
Kwa
miaka mingi sasa viongozi wanaopita katika klabu hizo wanakuja na ndoto za
kujenga viwanja, lakini zinayeyuka kutokana sababu mbalimbali ikiwemo
kuendekeza siasa kuliko vitendo.
Kwasasa
mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ana mkakati kabambe wa kujenga uwanja wa klabu
hiyo maeneo ya Jangwani, wakati huo huo, naye mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail
Rage akipambana na mpango kama huo maeneo ya Bunju jijini Dar es salaam.
Kwa
miezi miwili sasa, Uongozi wa Simba unaendelea na ujenzi wa uwanjao wake na
sasa umefikia hatua nzuri ya kuanza kutumika kwenye mazoezi ya klabu hiyo ikiwa
ni mara ya kwanza kumiliki uwanja katika historia yake.
Kutokana
na maendeleo hayo,uongozi wa Simba umewakaribisha wapenzi na wanachama wake
kesho Jumamosi katika Uwanja wao Bunju kwa
ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu.
Katibu
mkuu wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga amesema ujenzi huo ulioanza miezi miwili
iliyopita, unakaribia kukamilika na utakuwa uwanja wa kwanza rasmi wa mazoezi
wa klabu katika historia yake.
Vyombo
vya habari navyo vinaalikwa katika tukio hilo litakaloanza saa tano kamili
asubuhi.