ALIYETIWA MENO NA LUIS SUAREZ AFUNGUKA `MAZITO YA MOYONI`
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/aliyetiwa-meno-na-luis-suarez-afunguka.html
Tabasamu kubwa: Giorgio Chiellini ameumia na adhabu aliyopewa Suarez kwa kung`ata yeye.
BEKI wa Italia, Giorgio Chiellini amefunguka kutokana na adhabu aliyopewa Luis Suarez kwa kumng`ata.
Suarez amefungiwa na FIFA mechi tisa za kimataifa za Uruguay na miezi minne ya kutocheza soka.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool
aling`ata kwa mara ya tatu katika maisha yake ya soka baada ya
kumshambulia Chiellini wa Italia na kumtia meno katika dakika ya 80 ya
mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi na kushuhudia Uruguay ikishinda kwa
bao 1-0.

Suarez amefungia miezi minne kutocheza soka baada ya kumtia meno Chiellini
Lakini kwa Italia kuwa nje ya mashindano, Chiellini anaamini adhabu ya Suarez ni kali sana , hivyo anampa pole.
"Moyoni mwangu sina hisia za furaha,
kisasi wala hasira dhidi ya Suarez kutokana na tukio lile lililotokea
uwanjani na yamekwisha". Aliposti katika mtandao wake rasmi.
"Hasira zangu kwasasa zimebaki kwenye
mechi na matokeo. Ni wakati ambao namuwazia Suarez pekee na familia yake
kwasababu watakuwa kwenye wakati mgumu sana".

Hapa kitu cha meno tu: Suarez
(kushoto) alinaswa na Kamera akimng`ata beki wa Italia Giorgio Chiellini
(kulia) kwenye mechi ya jumanne.

Maumivu: Chiellini akivua jezi yake kuonesha sehemu aliyong`atwa na Suarez wakati wa mechi yao ya kundi D mjini Natal.
