SHEHENA YA VIROBA, VIPODOZI NA VYAKULA VILIVYOKWISHA MUDA WA MATUMIZI VYATEKETEZWA MKOANI MBEYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/shehena-ya-viroba-vipodozi-na-vyakula.html
Mamlaka
ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya za Rungwe na
kyela wamefanikiwa kukamata na kuteketeza shehena kubwa ya pombe haramu
aina ya viroba, vipodozi, dawa na vyakula ambavyo muda wake wa matumizi
umepita, bidhaa ambazo zimekamatwa wakati wa operesheni ya kutokomeza
uingizwaji wa pombe haramu za viroba mkoani mbeya.
Shehena
ya pombe haramu za viroba, vipodozi, vyakula na dawa ambazo muda wake
wa matumizi umekwisha vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20
vimeteketezwa kwa nyakati tofauti katika wilaya za rungwe na kyela,
zoezi ambalo limesimamiwa na kamati za ulinzi na usalama za wilaya hizo.
Mkuu
wa idara ya usafi na mazingira wilayani rungwe Dk. Nimroud kipoza na
afisa wa mamlaka ya mapato TRA wilayani kyela Paul Walalaze wanaelezea
madhara ya bishaa hizo kiafya na kiuchumi kwa watanzania.
Baadhi
ya vijana ambao wameunda kikundi cha kupambana na pombe haramu za
viroba pamoja na dawa za kulevya katika mpaka wa kasumulu wilayani kyela
wamesema mafanikio yao katika kudhibiti bidhaa hizo yanatokana na
kupata ushirikiano mzuri kutoka serikalini.
Meneja
wa mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa (TFDA) kanda ya nyanda za juu
kusini, Rodney Alananga amesema zoezi la kupambana na bidhaa hizo ni
endelevu, hivyo akawataka wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo
kuacha ili kuepuka kupata hasara.
