SEREY DIE AONESHA UZALENDO WA HALI YA JUU, AICHEZEA IVORY COAST LICHA YA KUFIWA NA BABA YAKE SAA MBILI KABLA YA MECHI YA COLOMBIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/serey-die-aonesha-uzalendo-wa-hali-ya.html
Huzuni: Serge Aurier, Cheick Tiote na Didier Zokora wote walijumuika na kiungo huyo wakati wa huzuni kabla ya mchezo kuanza
Siku ya huzuni: Shujaa Die aliichezea Ivory Coast saa chache baada ya baba yeka kufariki dunia
Die alijaribu kuimba wimbo wa taifa
lake, lakini kutokana na hisia kali alizokuwa nazo alishindwa kuzua
machozi yaliyokuwa yanambubujika.
Beki
Serge Aurier na mchezaji wa zamani wa Tottenham, Didier Zokora haraka walienda kumfariji mwenzao kabla ya mechi kuanza.
Nyota wa Newcastle, Cheick
Tiote pia alienda kumpa mkono wa pole Die, ambaye kwa bahati mbaya mechi yenyewe ameshuhudia nchi yake ikifungwa mabao 2-1.
James
Rodriguez na Juan Fernando Quintero waliifungia Colombia wakati
mchezaji wa zamani wa Asernal, Gervinho alifunga bao la kufutia machozi
kwa Tembo.
Die mwenye machungu ya kufiwa na baba yake alicheza mechi dhidi ya Colombia.