SERENGETI BOYS KUCHEZA AZAM COMPLEX
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/serengeti-boys-kucheza-azam-complex.html
Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya
Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti
Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos) itachezwa Ijumaa, Julai 18 mwaka huu katika
Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys ambayo imeingia moja kwa moja katika
raundi ya pili ya michuano hiyo inatarajia kuingia kambini wiki ijayo kwenye
hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Uwanja wa Karume jijini
Dar es Salaam, na itacheza mechi hiyo kuanzia saa 10 kamili jioni.
Amajimbos kama ilivyo Serengeti Boys imeingia moja
katika raundi ya pili pamoja na timu za Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso,
Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco, Nigeria,
Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Mechi ya marudiano itachezwa Afrika Kusini kati ya
Agosti 1na 3 mwaka huu. Iwapo Serengeti Boys itafuzu itaingia raundi ya tatu
itacheza mechi zake kati ya Septemba 12 na 14 mwaka huu wakati marudiano
itakuwa kati ya Septemba 26 na 28 mwaka huu.