SANTI CARZOLA SASA WASIWASI ARSENAL, ATLETICO MADRID WATEGA NYAVU ZAO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/santi-carzola-sasa-wasiwasi-arsenal.html
Santi Cazorla amesema atapima upepo wake katika klabu ya Asernal baada ya kombe la dunia.
Santi Cazorla akichuana na Sergio Busquets wakati wa mazoezi ya Hispania wiki iliyopita.
SANTI Cazorla amesema ataeleza hatima yake ya baadaye katika klabu ya Asernal mara kombe la dunia litakapomalizika.
Kiungo
huyo wa Hispania amekuwa akihusishwa na kuhama Emirates na anasemekana
kuwindwa na mabingwa wa La Liga na wanafainali wa UEFA, Atletico Madrid.
Carzola
ambaye kwasasa yupo na kikosi cha Hispania kinachojiandaa na mchezo wa
jumatano dhidi ya Chile, alijiunga na Asernal kutokea klabu ya Malaga
kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 16.5 mwaka 2012.
"Kombe la dunia litakapomalizika,
nitaanza kuwaza mazingira yangu," alisema Carzola alipokuwa anaongea na
gazeti za Hispania la AS.
"Sihitaji kuwaza kwa sasa na nimemwambia wakala wangu asiniambie chochote kama kuna ofa yoyote inakuja".