SAKATA LA NYOKA AINA YA CHATU JIJIINI ARUSHA,AWEKA MAMBO HADHARANI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sakata-la-nyoka-aina-ya-chatu-jijiini_20.html
Pichani ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu.
SAKATA
la kukutwa na chatu eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa
limechukua sura mpya baada ya mhusika kuhojiwa na mtandao wa jamiiblog
huu kuhusiana na tukio hilo.Aidha chatu huyo ambaye
alikutwa nyumbani kwa mmiliki huyo hivi karibuni imeelezwa tuhuma hizo
sio za kweli bali ni njama za kumuharibia tu na tukio hilo ni la
kutengenezwa na watu kwa lengo la kumchafulia jina lake.Magessa alisema
kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa safarini
yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio hilo na
kuwataarifu huyo chatu auawe.
.
Pia,
amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na
kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Aliongeza
kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao
ni kuwa wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa
mambo yote hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.Magessa
alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na taarifa mbalimbali ambazo
zimekuwa zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao juu ya
tukio hilo ila yeye amenyamaza kimya na amemwachia Mungu kwani ndiye
ajuaye kila kitu.I
KUHUSU KUTENGWA KWAKE KANISANI .
Aidha
akizungumzia kuhusiana na swala la kutengwa kwake na Kanisa katoliki
alisema kuwa huo ni uongo na uzushi hakuna kitu kama hicho kwani
wanamwelewa vizuri sana tabia yake na kuwa hana tabia ya ushirikina.
‘Tena
waumini wa kanisa katoliki watakuja kufanya jumuiya nyumbani kwangu na
tayari kuna masalaba pale kama kweli ningekuwa nimefanya hivyo leo hii
wangefuata nini hapa kanisani’alisema Magessa.
Naye
mkewe Selina Magessa , akizungumza na jamiiblog kuhusiana na tukio hilo
alisema kuwa.tangu ameanza kuishi na mumewe miaka mingi hadi sasa hivi
,hajawahi kusikia wala kuona
vitendo vya ushirikina.
“Niko na
mume wangu miaka mingi, sijawahi kusikia kuwa anafuga nyoka ndani wala
sijafiwa na mtoto yeyote, wote watatu wapo ila nashangaa kusikia kauli
kwamba mume wangu aliagiza nyoka asiuawe kwa kuwa ni mtoto wake ama mama
yake mzazi,” alisema Selina.
Alisema
kuwa , kwa sasa hivi ni muda wao kupumzika na kutafakari mambo yao sio
wakati wa kuzungumzia swala hilo tena kwani wamechishwa na maneno kila
mahali ili wanachofanya ni kumwachia mungu pekee ndiye ajuaye.
Hata
hivyo ,Magessa anapenda kuwaelezea watanzania kwamba huyo chatu sio wa
kweli ni wa kurushwa kwenye fensi yake ili amchafulie kwani chatu wa
ukweli asingeweza kuburuzwa hadi kanisani kwani kila mtu anamwelewa
mnyama huyo jinsi alivyo mkali ,kwa hiyo hizo ni njama tu za kuharibiana
kwenye maisha .
Hivyo alisema kuwa, kusisitiza kuwa anaombwa watanzania wamwelewe kwani chatu wa ukweli wanafahamika.
ATOA RAI KWA VYOMBO VYA HABARI.
Aidha
alivitaka vyombo hivyo kuelimisha jamii badala ya kupotosha ukweli wa
jambo kama ambavyo sakata hilo limezua sura tofauti kwa watanzania .
‘mnajua
nyie ndio vyombo tunavyovitegemea kwa jamii ,sasa mkiandika vitu
ambavyo hamna uhakika navyo mnategemea italeta picha gani kwa jamii ya
watanzania ‘alisema Magessa.(CHANZO Pamela Mollel jamiiblog)