ROSE MUHANDO KUZINDUA FACEBOOK AGOSTI 3/2014
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/rose-muhando-kuzindua-facebook-agosti.html
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi
wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza
Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu ka FACEBOOK ya
mwimbaji wa muziki wa injili anayevuma Rose Muhando utakaofanyika kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee Agosti 3 /2014 jijini Dar es salaam, ambapo
amesema baadhi ya mapato yatakwenda kuviwezesha mitaji zaidi ya vituo 10
vya watoto yatima jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua zaidi kwa
waandishi kuhusu uzinduzi huo unaoarajiwa kuwa mkubwa katika ukanda wa
Afrika Mashariki.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akiwaeleza zaidi
waandishi na kusema taarifa zaidi zitaendelea kutolewa ili kuwajulisha
mashabiki wa muziki wa injili juu ya uzinduzi huo.