PICHA:BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR MWENYEJI WA MKUTANO WA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA USAJILI WA CHAKULA NA DAWA KWA NCHI ZA EAC.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/pichabodi-ya-chakula-dawa-na-vipodozi.html
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi akifungua Mkutano wa siku
mbili wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa kufanya tathmini ya utekelezaji
wa usajili wa Chakula na Dawa kwa Mamlaka za udhibiti wa bidhaa hizo kwa
Nchi wanachama.

Afisa
wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Bi. Hidaya Juma Hamad
akielezea changamoto wanazokabiliana nazo katika utekelezaji wa kazi za
Bodi hiyo, (kusho) ni Meneja Operesheni wa Mradi wa Usajili wa chakula
na Dawa wa nchi za Afrika Mashariki Apolo Muhaiwira.

Mrajis
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Dkt. Burhani Othman Simai
akijibu masuali aliyoulizwa na wajumbe wa Mkutano huo, (kushoto)
Mwenyekiti wa Mkutano Dkt. Jamala Adam Taib.

Mratibu
wa Mradi wa Usajili wa Chakula na Dawa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Bw. John Patrick (aliesimama) akitoa maelezo kuhusiana na Mradi huo
katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Grand Palace Mjini Zanzibar.

Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi (wakatikati) waliokaa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano wa Jumuiya ya Africa Mashariki wa
tathmini ya utekelezaji wa usajili wa Chakula na Dawa uliofanyika Hoteli
ya Grand Palace Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar
