PENZI LA RAY NA JOHARI...MASHABIKI WAFUNGUKA KIIVI...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/penzi-la-ray-na-joharimashabiki.html
Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’
MASHABIKI wa
sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa
kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na
Blandina Chagula ‘Johari’.Ishu
hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa
mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde
Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.Mashabiki
walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe
wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.