NZIA:- MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO KWA KUANGUKIWA NA KICHUGUU {PICHA}
Mwili wa Mkazi wa kijiji cha Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera Raulian Ladislaus mwenye umri wa Miaka 40, u kiwa umeangukiwa na Ki...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/nzia-mtu-mmoja-afariki-dunia-papo-hapo.html
 |
|
Mwili wa Mkazi wa kijiji cha
Ruganzo wilayani Ngara mkoani Kagera Raulian Ladislaus mwenye umri wa Miaka 40, ukiwa umeangukiwa na
Kichuguu na kufariki papo hapo June 12,2014,mchana wakati akichimba kichuguu
hicho kwa lengo la kuangamiza mchwa waliokuwa wakiharibu miwa yake aliyoilima karibu kichuguu hicho.
|
 |
|
Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 asubuhi wakati Marehemu
akichimba kichuguu hicho ili kukihamisha kwa lengo la kusalimisha ekari moja ya
Miwa iliyokuwa karibu na kichuguu hicho kabla ya kuangukiwa na kukandamizwa na
Kichuguu hicho kifuani.
|
 |
|
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji
cha Uganzo walishirikiana kuchimba kichuguu hicho kwa lengo la kumtoa marehemu
ambaye alizikwa juzi June 12, 2014,Jioni Nyumbani Kwake.. ‘’Mungu ailaze mahali pema peponi.... Amina..’’
|