Flatnews

Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao


Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao
Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer) amezungumzia uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Msami alizunguka sana mbuyu kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara ya kwanza aliamua kuiambia tovuti ya Times Fm kauli yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.
“Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha.” Amesema Msami..
Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba Msami ni mkubwa kwa Uwoya. Chukua hiyo!
“Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti Boy’ kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu Serengeti Boy.
“Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya.” Alisisitiza Msami 
Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.
Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika kuu na kwamba ni filamu ambayo itahusisha dance na muziki. Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.
“Movie inakuja very soon, watu wakae tayari.” Amesisitiza.

Post a Comment

emo-but-icon

item