Mwanamke wa Sudan aliyefungwa jela kutokana na kuolewa na mume mkristo
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mwanamke-wa-sudan-aliyefungwa-jela.html
Headlines
za dunia pia zimegonga sana kwenye siku hizi za karibuni kuhusu
mwanamke wa Sudan ambae amekua akisubiria hukumu ya kunyongwa kwa kosa
la kuolewa na mume mkristo huku dini ya baba yake ikiwa inajulikana wazi
kwamba ni Muislamu.Wizara ya mambo ya nje nchini Sudan imesema
kuna uwezekano wa Meriam kuachiwa huru ndani ya siku kadhaa zijazo hivyo
hukumu ya kifo inayomkabili inaweza isiwepo manake Sudan ni nchi
inayoheshimu uhuru wa watu kuabudu.
Hukumu
hiyo aliipata baada ya kugoma kubadili dini na kurudi kwenye Uislamu
ambao ni dini ya baba huku mama yake aliemlea akiwa ni Mkristo.
Meriam
ambae yuko kwenye ndoa na Daniel Wani tangu mwaka 2011, alijifungua
mtoto wake wa pili akiwa gerezani Jumatano iliyopita ambapo vyombo vinne
vya habari vya kimataifa vimeripoti kwamba alijifungua akiwa bado na
minyororo
Wakili wa Ibrahim pamoja na mumewe Daniel wamesema hawajafahamishwa chochote kuhusiana na mipango ya kumwachilia huru.
Mahakama
ilisema Meriam angeweza kumuhudumia mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya
hukumu yake kutekelezwa ambapo taarifa nyingine ya juzi ilisema
Mwanaume huyu amepewa ruhusa ya dakika ishirini kila wiki kwenda kumuona
mke wake gerezani.
Unaambiwa nchi ya Sudan ina idadi kubwa ya Waislam na sheria za kiislamu zimekuwa zikipewa uzito tangu mwaka 1980.