MHE. MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA CHINA, CUBA, JAPAN, MSUMBIJI NA KAIMU BALOZI WA UJERUMANI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mhe-membe-akutana-kwa-mazungumzo-na.html
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.)
akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Youqing
alipofika kwa ajili ya mazungumzo ambayo yalihusu pia ziara ya Makamu
wa Rais wa China atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 26
Juni, 2014.
Mkurugenzi
Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na
Balozi LU (hawapo pichani)
Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Cuba
Mhe.
Waziri akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe.
Jorge Luis Lopez Tormo alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu
kuimarisha ushrikiano kati ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba
zinashirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na siasa.
Mhe. Membe akimsikiliza kwa makini Balozi Tormo.
Mazungumzo yakiendelea huku Afisa Mambo ya Nje, Bw. Lucas Mayenga akinukuu.
Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Japan
Mhe.
Membe akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.
Masaki Okada alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha
ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Mhe. Balozi Okada akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe.
Mkurugenzi
Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nathaniel Kaaya akifuatili
mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Okada (hawapo pichani)
Mkutano wa Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani
Mhe.
Membe akimkaribisha ofisini kwake Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini,
Bw. Hans Koeppel alipofika kwa mazungumzo na Mhe. Waziri kuhusu salamu
za shukrani kwa Serikali ya Tanzania kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje
wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeir kufuatia ziara yake ya
mafanikio aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi 2014
Mhe. Membe akipokea barua ya salamu hizo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akifuatilia mazungumzo kati
ya Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini (hawapo pichani)
Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Msumbiji
Mhe.
Membe akizungumza na Balozi wa Msumbiji hapa nchini, Mhe. Vicente M.
Veloso alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha
ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Veloso na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao.