Messi amfunika Ronaldo vibaya
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/messi-amfunika-ronaldo-vibaya.html

Lionel
Messi ni mchezaji mwenye thamani kubwa duniani kutokana na kulipwa
karibu mara mbili zaidi ya Cristiano Ronaldo anayemfuatia....
Hiyo ni kwa sababu umri wa Messi ni miaka 26 wakati Ronaldo ana miaka 29.
Pia
Raheem Sterling ni mchezaji mdogo (19) na mkubwa ni Andres Iniesta (30)
walioingia katika orodha hiyo ya wachezaji 25 wanaolipwa zaidi kwenye
fainali za Kombe la Dunia.
Utafiti
huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Uswisi kiitwacho Neuchatel kwa
kushirikiana na OptaPro, uliangalia thamani za wachezaji wa ligi tano
kubwa za Ulaya kwa kutazama mishahara yao na gharama za uhamisho.
Messi kwa
sasa ana thamani ya Pauni 175.6 milioni za Kiingereza akifuatiwa na
Cristiano Ronaldo mwenye thamani ya Pauni 92.7 milioni za Kiingereza
huku Eden Hazard akishika nafasi ya tatu kwa thamani ya Pauni 66.7
milioni,
Wachezaji
23 kati ya 25 walioshika nafasi za juu kwenye tafiti hiyo ni
washambuliaji. Walobaki ni viungo wakabaji ambao ni Sergio Busquets na
Paul Pogba.
Katika
kundi hilo la wanasoka 25, 11 wanatoka Ligi Kuu ya Uingereza, nane
wanacheza Hispania huku Ufaransa, Ujerumani na Italia zikitoa wachezaji
wawili kila mmoja.
Katika
soko la juu la nyota hao 11, Ronaldo na Gareth Bale (Pauni 51.2m)
wamenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi kwani Messi hajahama Barcelona toka
ajiunge nao.
Kyle
Walker na Luke Shaw pia wameingia katika kikosi cha wachezaji 11 wenye
thamani zaidi duniani, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na CIES
Football Observatory.