MBASHA ATOSWA GEREZANI KEKO, AKESHA AKILIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mbasha-atoswa-gerezani-keko-akesha_1327.html
Basi lililombeba Emmanuel Mbasha likiwa chini ya ulinzi mkali wa askari magereza likisindikizwa kuelekea mahakamani.
Jina zima
ni Emmanuel Mbasha (32) ambaye ni mume wa mwimba Injili Bongo, Flora
Mbasha juzi amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar
es Salaam ishu ni yale madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina
lipo).Akisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,
Wilberforce Luago, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mshitakiwa
huyo alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata- Kimanga jijini Dar es
Salaam.
Katika
shitaka la kwanza, Wakili Katuga alisema Mei 23, mwaka huu, huko Tabata-
Kimanga jijini Dar, mtuhumiwa huku akijua ni kinyume cha sheria
alimwingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa ni shemeji yake.
Katika
shitaka la pili, wakili huyo alisema Mei 25, mwaka huu hukohuko Tabata
Kimanga, mshitakiwa alimwingilia tena kwa nguvu shemeji yake huyo huku
akiendelea kujua ni kinyume cha sheria.
MBASHA AULIZWA, ATOA NENO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alipotakiwa kusema kweli si kweli mahakamani hapo, alisema si kweli.
SERIKALI YASEMA HAINA PINGAMIZI YA KUWA HURU
Baada ya kutamka neno hilo, upande wa Jamhuri ulitoa hoja kwamba
hauna pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa hivyo, Hakimu Luago alitaja
masharti ya dhamana kwa mshitakiwa.
Hakimu
huyo alisema ili mshitakiwa awe huru kwa dhamana alitakiwa kuwa na
wadhamini wawili. Mmoja kati ya wadhamini hao awe mfanyakazi wa
serikalini, mwingine atoke kwenye taasisi inayotambulika. Wote kama
wapo, walitakiwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 5 kwa kila
mmoja.
MBASHA AENDA KEKO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana
hiyo hivyo hakimu aliamuru apelekwe kwenye Mahabusu ya Keko jijini Dar
ambako atakuwa chini ya ulinzi. Mbasha aliondolewa mahakamani hapo akiwa
chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kwa mujibu wa habari kutoka mahabusu, juzi baada ya kufikishwa
magereza, mtuhumiwa huyo alikesha akilia na kusali ili janga hilo
limwepuke, lakini si kama atakavyo yeye bali mapenzi ya Mungu yatimizwe.
LEO ANARUDI TENA
Ni kama shughuli imeanza kwani, hakimu alisema leo (Juni 19)
mshitakiwa alitakiwa kurudi tena mahakamani hapo ambapo kesi yake
itatajwa tena.
FLORA ANAPOKEAJE TAARIFA ZA MUMEWE?
Paparazi alimsaka Flora ili azungumzie madai ya mumewe kupandishwa
mahakamani ambapo alisema hana mawasiliano kabisa na Mbasha kwa hiyo
hajui chochote kuhusu habari hizo.
PAPARAZI: “Sasa ndiyo unaambiwa, wewe unazipokeaje taarifa hizo?”
FLORA: “Hizo habari sizijui kama nilivyosema.”
Jumatatu
iliyopita, paparazi aliipiga namba ya Mbasha, simu ilipokelewa na mtu
mwingine ambaye alipoulizwa alipo Mbasha, alijibu hayupo kisha akakata
simu.
Baada ya hapo, kila paparazi alipopiga simu hiyo haikupokelewa mpaka siku ilipoisha.
Jumanne iliyopita kabla Mbasha hajapanda kizimbani, paparazi alipiga
tena simu hiyo ikapokelewa na mtu yuleyule wa jana yake lakini safari
hii akawa mvumilivu, kwani hakukata simu haraka. Mazungumzo yalikuwa
hivi;
paparazi: “Kaka habari yako?”
MPOKEA SIMU: “Njema, nani mwenzangu?”
paparazi: “Mimi ni … , naweza kuzungumza na Mbasha?”
MPOKEA SIMU: “Mbasha huwezi kuzungumza naye kwa sasa, ametoka.”
paparazi: “Saa ngapi atakuwa amerudi?”
MPOKEA SIMU: “Mwenyewe akiwa tayari atakupigia, nitamwambia.”
paparazi: “Oke, sawa.”
Flora Mbasha na mumewe.
NI KASHFA YA AINA YAKE
Sakata la Mbasha, liliibuliwa na kashfa kwamba mume huyo alimbaka
mara mbili shemeji yake huyo ambaye alitoa taarifa kwenye Kituo cha
Polisi Tabata Shule jijini Dar.
Hata hivyo, polisi walipokwenda kumkamata nyumbani kwake hawakumkuta
na baada ya hapo alitoweka jumla mpaka Jumatatu iliyopita ambapo
inadaiwa alikuwa akiishi kwa mdogo wake, Mbezi, Dar.
Kashfa
hiyo ndiyo iliyoibua tuhuma kutoka kwa Mbasha akisema kuwa Mchungaji
Gwajima alimuhifadhi mkewe nyumbani kwake baada ya yeye kukumbwa na
tuhuma hiyo ya kubaka madai ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliyapangua
vizuri na Flora akabainika kwamba anaishi hotelini, Sinza jijini Dar.


