Flatnews

MATUKIO KATIKA PICHA NDANI YA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


UT4Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano wa TASAF  Bw. Zablon Bugingo, , Afisa Mifumo, Bi. Desderia Bomba –Misa, Mtaalam wa Mawasiliano, Bibi. Zuhura Mdungi, Afisa Mapokezi Bi. Jenny Solomon na Mtaalam Msaidizi wa Uchapishaji Bw. Victor Manyai wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
UT1Baadhi ya wananchi wakifuatilia maelezo kutoka kwa Wafanyakazi wa TASAF wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

UT2Afisa Mifumo wa TASAF Bi. Desderia Bomba –Misaakitoa maelezo kuhusu Miradi inayotekelezwa na TASAF Awamu ya Tatu  kwa  mwananchi aliyetembelea banda lao wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,mwenye fulana nyeupe  kushoto ni Mfanyakazi wa Mapokezi wa TASAF Bi. Jenny Solomon.
UT3Mtaalam Msaidizi wa Uchapishaji Bw. Victor Manyai akimkabidhi baadhi ya machapisho ya TASAF mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la TASAF katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mfanyakazi wa Mapokezi wa TASAF Bi. Jenny Solomon.
Picha na Frank Shija, WHVUM

Post a Comment

emo-but-icon

item