Maskini Penny achungulia kaburi...pata undani kamili.
MTANGAZAJI wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa ugonjwa uliompiga juzikati ulikuwa ‘serious’ kiasi cha ...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/maskini-penny-achungulia-kaburipata.html
MTANGAZAJI wa
maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa
ugonjwa uliompiga juzikati ulikuwa ‘serious’ kiasi cha kuona ni Mungu tu
amemwokoa.
Mtangazaji wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akiwa hoi hospitaliakisumbuliwa na ugonjwa wa Athma.
Akichezesha
taya na paparazi wetu, Penny alisema anamshukuru Mungu anaendelea
vizuri kwani alikuwa na hali mbaya baada ya kubanwa na ugonjwa wa Athma
kwa siku tatu nzima akiwa anasaidiwa kupumua na mashine ya oxygen.
Mtangazaji maarufu
wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akisaidiwa kupumua na mashine
ya oxygen baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Athma.
“Ukweli
nilikuwa na hali mbaya huwa nasumbuliwa na Athma mara kwa mara lakini
naweza kubanwa kwa siku moja ila ya safari hii imekuja kwa nguvu sana
kwa sababu ilikuja na mafua makali jambo lililosababisha nilazwe kwa
siku tatu katika Hospitali ya AAR huku nikipumua kwa kutumia mashine,
kweli Mungu ni mkubwa, ninaendelea vizuri,” alisema Penny.