Malik:Serikali ya umoja haifai Iraq
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/malikserikali-ya-umoja-haifai-iraq.html
Waziri mkuu nchin Iraq Nouri al
Malik ameonya kwamba kubuni serikali ya umoja nchini humo ni mapinduzi
dhidi ya katiba ya taifa hilo,na kuwa itaharibu mfumo wa demokrasia
uliwekwa kufuatia kung'atuliwa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa taifa
hilo marehemu Saddam Hussein miaka kumi na moja iliopita.
Marekani na mataifa mengine wamekuwa
wakimshinikza waziri huyo mkuu kubuni serikali itakayoshirikisha wote
kufuatia uchaguzi mwezio Aprili huku watu wa dhehebu la kisunni walio
wachache na wale wa kikurdi wakiwakilishwa.
Nouri al Malik
Lugha nzito aliyotumia kupinga wazo la serikali ya kitaifa wakati ambapo kuna tishio la wapiganaji wa kisunni ni onyo kubwa.
Bwana malik anaweka wazi kwamba atabuni serikali ya chaguo lake kwa kuwa ana haki kulingana na katiba kufuatia uchaguzi wake wa mwezi Aprili ambapo chama chake kilishinda kwa kura nyingi.
Matamshi yake yanaonyesha uwezekano kwamba serikali yake mpya ambayo nisharti ibuniwe mnamo mwezi Agosti haitakuwa ya uwakilishi kama inavyoshinikizwa na Marekani.
