Flatnews

Makali ya magonjwa, kero duniani



Betty Baiga anaugua Saratani ya Matiti na uchungu aliopitia anasema hausemeki
Kukosekana kwa fursa ya kupata dawa za kupunguza uchungu au makali ya magonjwa yasiyo na tiba kwa wagonjwa mahututi ni ''jambo ambalo linapuuzwa sana,” wasema wataalamu.
Takwimu zinaonyesha kuwa watu milioni 18- hasa kwenye mataifa yanayokua- walikufa kutokana na uchungu ambao ungezuilika mwaka wa 2012, huku kukiripotiwa kuwa wagonjwa wa Saratani nchini Ethiopia walijirusha mbele ya malori ili kuepuka uchungu.
Shirika la kimataifa la 'Palliative Care' limesema kuwa sehemu ya tatizo ni kukataa kwa serikali mbalimbali kuwapa wagonjwa fursa ya kupata madawa ya kupunguza uchungu vya makali kama vile Morphine.
Unaongeza kuwa vikwazo vimewekwa kwa hofu ya wagonjwa kutawaliwa na madawa hayo.
Mwezi uliopita, maafisa wa afya kutoka mataifa yapatayo 200 walikutana katika makao ya UN na kuahidi kuipa kipaumbele mpango wa kupunguza makali kwa wagonjwa wenye maradhi yasiyotibika.
Betty alihisi uchungu kwa muda mrefu bila kusaidiwa
Hii ndio mara ya kwanza utaalamu huu kutambuliwa na kuenziwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Betty Naiga mwenye umri wa miaka 48, aliyepimwa na kupatikana na ugonjwa wa saratani na ambaye ni mkazi wa kijiji kidogo cha wilaya ya Wakiso nchini Uganda, analala kwenye godoro dogo sakafuni katika chumba chake kidogo cha manjano.
Betty aliishi kwa uchungu hadi alipokutana na Allen, mhudumu wa kujitolea katika huduma za kuwasaidia wagonjwa wenye magonjwa yasiyo na tiba kutoka hospitali ya Afrika Uganda.
'Mateso'
Baada ya hospitali hiyo kujihusisha na afya yake, Betty alipata fursa ya kupata matibabu ya Chemotherapy na kwa hivyo akahitaji dawa ya kupunguza makali ya Morphine.
''Maisha yangu yamebadilika pakubwa sana tangu nilipoanza kupata matibabu. Madawa yalisaidia kupunguza maumivu yangu,” alisema Betty.
Uganda inaongoza barani Afrika kwa huduma hizi za kuwasaidia wagonjwa mahututi.
Betty alifainikiwa kupata usaidizi wa shirika moja la kibinafsi lililompa madawa ya kupunguza makali ya ugonjwa wake
Taifa hilo linajitengenezea madawa ya majimaji ya Morphine kwa kutumia mchanganyiko wa unga wa morphine na maji. Hata hivyo, mataifa mengine yanayoendelea yana usambazaji mdogo wa madawa haya.
Mataifa mengine kama vile Libya na Afganistan, hayapeani huduma hizo za kutuliza maumivu.
Huko Pakistani, zaidi ya watu 350000 walihitaji aina hii ya huduma katika mwaka wa 2012, lakini walioweza angalau kuipata ni takriban 300 tu, kulingana na takwimu zilizoonyeshwa BBC.
Kulingana na WPCA, kuna tu huduma mbili kama hizo zinazotolewa katika nchi hiyo nzima.
Huduma moja iliyoko Msumbiji iliwasaidia watu 153 pekee, kati ya 100,000 walihitaji huduma hiyo ya kupunguza makali katika mwaka wa 2012.

Post a Comment

emo-but-icon

item