Flatnews

Majibu Ya Nay Wa Mitego Kuhusu Tuhuma Za Kuiba Wimbo wa Wababa


Nay wa Mitegoo

Ijumaa iliyopita, Wababa ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya kuimba ya Bongo Star Search aliwalalamikia maswaiba Nay wa Mitego na Diamond Platinumz kwa wizi wa kazi zake kwa wakati tofauti na njia tofuati alipoongea katika Friday Night Live ya East Africa Radio.
WababaWababa alidai Diamond amemuibia wimbo wake wa Kitorondo ambao aliufanya na Dogo Aslay miaka karibu minne iliyopita na akafanya hadi video na iko kwenye mtandaoni.


Lakini pia alimtuhumu Nay wa Mitego kwa kupanga njama za kutaka kumuibia wimbo wake aliomshirikisha ndani ya Mazoo records ambapo Nay wa Mitego anadaiwa kumtafuta Mazoo kimya kimya na kutaka kumlipa mkwanja ili amkabithi wimbo huo kinyamela na kumtosa Wababa.
The True Boy himself amefunguka kuhusu Tuhuma za Wababa:
“Sijui niongee nini kuhusu hii issue…mimi nimeisikia. Lakini mimi napenda beat nzuri, mimi sijataka ile beat. Lakini kilichofanyika ni kwamba producer ametaka kunipa mdundo wa design ile lakini sielewi ni kwa nini tena maneno yamekuja kwamba mimi nimetaka kuilipia ile beat. No, mimi nilisema 


napenda ule mdundo wa design ile kwa gharama yeyote naweza nikaulipia lakini sio kama nimetaka mdundo wa dogo..no.
“Ngoma ya dogo nzuri, mimi mwenyewe nimependa the way nilivyoimba lakini sio kama nitake ngoma yake au beat yake hapana ntakuwa nakosea, nitakuwa nakosea sana. Lakini mimi nilichoongea ni tofauti na hicho labda wale wameninukuu vibaya. Mwisho wa siku naweza kusema mimi siwezi…kwanza muziki wangu watu wanaujua uko tofauti sana. Hiyo ngoma yenyewe ukiisikia iko tofauti sana, na mimi nimetaka changes kwenye muziki wangu.. nilimwambia producer nataka beat ya design hii ambayo inaweza kuwa kali zaidi ya hii na mimi nikailipia hela yoyote unayoitaka. Kwa hiyo mwisho wa siku sijui nini kiliendelea hapo katikati.
“Si kweli…ni nyimbo nzuri kweli mimi niliipenda niliisifia na ndio maana nilikuwa na nguvu ya kuweza kuifanya naweza kusema kwa asilimia mia moja. Mimi sijafanya featuring tangu mwaka jana. Kwa mwaka huu nilifanya featuring mbili tu,  nilifanya ya kwanza ya Kala Jeremiah na hii ni ya pili tena baada ya kutumiwa demo nikaoni ni nzuri sana. Niliifanya kwa nguvu kwa sababu niliona ni nyimbo nzuri ambayo hata mimi mwenyewe watu wanaweza kuendelea kusema ‘okay mwana amefanya collabo nzuri’. Siwezi kuchukua nyimbo yake yeye, nyimbo yake yeye.
“Mimi anitafute, siku mbili tatu hizi nilikuwa busy na mambo yangu. Nilikuwa namalizia nyumbani kwangu huku na kule vitu vingi shows na vitu vingine. Anitafute tutaongea. Mimi naweza kusema hivi ni mdogo wangu, hakuna ambacho kitaharibika lakini sidhani kama itaweza kufikia hatua tukagombana mimi na yeye. Labda yeye alininukuu vibaya.”

Post a Comment

emo-but-icon

item