MAJI KERO KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MPANDA NDOGO, WASAFIRI KILOMITA MBILI KUPATA HUDUMA
Wanafunzi wanahitaji kisima cha maji Mpanda
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/maji-kero-kwa-wanafunzi-wa-shule-ya.html
Shule
ya Msingi Mpanda ndogo katika halmashauri ya wilaya ya
Mpanda inakabiliwa na changamoto ya maji hali inayowalazimu wanafunzi
kufuata maji kwenye mto uliopo kijini cha jirani kilicho umbali wa kilomita 2.
kufuata maji kwenye mto uliopo kijini cha jirani kilicho umbali wa kilomita 2.
Hayo
yameelezwa na walimu wanaofundisha katika shule hiyo
walipokuwa wakizungumza na mbunge wa jimbo la mpanda Vijijini , Moshi
Kakoso aliyefanya ziara shuleni hapo hivi karibuni na kupata nafasi ya
kuzungumza na walimu kupata changamoto zinazowakabili pamoja na kukagua
maendeleo ya miradi inayotekelezwa.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkuu wa shule hiyo, Rashidi Msyete alieleza
changamoto mbalimbali zinazoikabili shule ikiwemo utoro kwa kwa baadhi
ya wanafunzi,uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi , shule kutokuwa na
mlezi hasa kwa wanafunzi wa kike (Matroni).
Alisema
kutokana na kukosa maji wanafunzi inawalazimu kuvunja masomo na kufuata
maji umbali mrefu hali inayowafanya kupoteza muda mwingi nje ya vipindi vya madarasani.
Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo walimwomba mbunge kusaidia kwa njia moja au nyingine kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
Kwa
upande wake mbunge Kakoso aliagiza kamati ya maendeleo ya Kata kukaa
na uongozi wa Halmashauri kuangalia kwenye mfuko wa jimbo ambalo upo kwa
ajili ya kusaidia maendeleo katika jimbo waletewe maji ikiwa ni pamoja
na kuchimbiwa kisima katika shule hiyo ili kuondoa kero hiyo.
