MAINDA: ATA MKINISEMA NA KUNICHEKA SIACHI ULOKOLE NG`OOOO
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya y...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mainda-ata-mkinisema-na-kunicheka.html
Staa
wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa
hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya
wokovu.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza
na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata shida sana
kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu wanachukulia
ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu
ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza
vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa
jicho linginewanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya
kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si
mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda.