Flatnews

MAADHIMISHO YA SIKU YA SIKO SELI DUANIANI YAFANYIKA DAR KWA UZINDUZI WA KILINIKI YA WATOTO.


  Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk Sarah Maongezi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kliniki ya watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani yalifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maabara, Dk. Alex Magesa, Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey na Mkurugenzi waTiba wa Hospitali ya Muhimbili, Dk Hedwiga Swai na kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Eligius Lyamuya..
 Mkurugenzi wa Idara ya Uboreshaji Afya wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk Sarah Maongezi akihutubia wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana.
 Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania (TSCF), Grace Rubambey akitoa takwimu kuhusu hali ya ugonjwa nchini. Tanzania ni nchi ya tano kuwa na wagonjwa wengi duniani ambao karibu watoto 11,000 huzaliwa na sikoseli kila mwaka.
 Mmoja wa wasichana wanaougua sikoseli, Hafsa Omari akitoa ushuhuda wa maisha yake na ni jinsi gani mtu anayeugua ugonjwa huo anaweza kuishi maisha salama.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati) pamoja na wageni wengine wakipata maelezo kuhusu kliniki ya watoto kutoka kwa Dk. Elisha Osati muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa kliniki hiyo.
  Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati) pamoja na wageni wakipata maelezo kuhusu kliniki ya watoto kutoka kwa Dk. Elisha Osati muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa kliniki hiyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Sikoseli Duniani, Dk. Sarah Maongezi (katikati, mstari wa mbele) pamoja na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya watoto wanaougua sikoseli wakiwa na wazazi na wanafamilia wengine wakati wa maadhimisho hayo.
 Msanii wa muziki wa kufokafoka, Hudu Juma Mpili ambaye pia anaugua sikoseli akitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa maadhimisho.
chanzo jiachie blog.

Post a Comment

emo-but-icon

item