LOWASSA ATABIRI BOMU KULIPUKA TANZANIA
Waziri Mkuu Mstaafu Mh Edward Lowassa.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/lowassa-atabiri-bomu-kulipuka-tanzania.html
Jana,
Lowassa kuongezeka kwa makundi ya vijana wanaopora watu katika maeneo
mbalimbali nchini ni ishara ya ukosefu wa ajira. “Watanzania sasa tupo
milioni 48 na kila mwaka vijana zaidi ya 30,000 wanahitimu vyuo vikuu na
kazi hakuna, pamoja na hilo hatuambiwi ni vijana wangapi ambao hawana
kazi,” alisema Lowassa.
Alisema
lazima Serikali itengeneze ajira kwa wananchi wake, huku akimtolea mfano
Rais wa Marekani, Barack Obama kwamba alishinda awamu ya pili kwa
sababu ya kutengeneza ajira.
“Mfano
mzuri ni katika uanzishwaji wa viwanda. Tunapofikiria kuanzisha kiwanda
cha pamba kwanza lazima tuangalie tutatengeneza ajira ngapi,” alisema.
Katika
kuonyesha kuwa ajira sasa ni tatizo nchini, juzi jioni wakati wa mjadala
wa Bajeti Kuu, Naibu Spika Job Ndugai alisema Mtanzania mwenye nia ya
kugombea urais mwaka 2015 ili aweze kuelekewa kwa wananchi ni lazima
aeleze mikakati ya kuwasaidia vijana kupata ajira.
“Ajira ni
tatizo kubwa na lazima lishughulikiwe. Kuna vijana hawaendi shule
lazima watazamwe. Kuna wanaomaliza darasa la saba, kidato cha nne, cha
sita na vyuo vikuu. Nazungumza kutoka moyoni kabisa. Hizi ni dakika za
mwisho za Serikali ya awamu ya nne, wale wanaojipanga kwa awamu ya tano
kama hawataongelea ajira basi waandike wameumia.”
Ndugai
alisema vijana wasio na kazi ndiyo wapigakura wakubwa na kusisitiza kuwa
mgombea yeyote makini ni lazima afikirie suala la ajira kwa vijana.