KUHUSU MAREKANI KUIWEKEA VIKWAZO UGANDA BAADA YA KUPITISHA SHERIA KUPINGA USHOGA.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kuhusu-marekani-kuiwekea-vikwazo-uganda.html
Marekani imeiwekea Uganda vikwazo
kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsia moja katika taifa
hilo.Inasema vikwazo hivyo vitajumuisha marufuku ya wanaharakati
waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Ikulu ya nchi hiyo pia imesema
itapunguza misaada kwa miradi kadhaa inayofanya kwa msaada wa Marekani
kwa mamlaka za Uganda na kufuta mazoezi ya kijeshi kati ya Uganda na
Marekani.
Uganda imesema haitashinikizwa na
nchi za Magharibi kwa ajili ya kubadilisha sheria zake zinazowafanya
watakaokutwa na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kufungwa jela
maisha.
Sheria hiyo iliyosainiwa mwezi
February inaruhusu kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na hatia ya
kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kufanya kuwa uhalifu vitendo vyote
vinavyohusiana na mapenzi ya jinsia moja