Flatnews

KOCHA SPAIN AMTIMUA FABREGAS MAZOEZINI

FABREGAS NA DEL BOSQUE


FABREGAS NA DEL BOSQUE
Kiungo mpya wa Chelsea, Cesc Fabregas amezozana na kocha wake Vicente del Bosque ambaye amechukua uamuzi wa kumtimua.
Hali hiyo imetokea mazoezini leo kwa wawili hao kuzozana wakati Hispania ikiwa imevuliwa ubingwa na inasubiri kucheza mechi dhidi ya Australia ambayo ni kujiburudisha tu.


AKIMKABIDHI BIB XAVI KABLA YA KUTOKA NJE

Hispania imefungwa mechi mbili kwenye kundi lake dhidi ya Hispania na Chile na Fabregas ambaye ametua Chelsea akitokea Barcelona alicheza ile dhidi ya Uholanzi tena dakika za mwisho.
Inaonekana hajafurahia kubaki benchi hali iliyosababisha mzozo huo.
Licha ya juhudi za wachezaji wengine kuzuia mzozo huo, Fabregas alionekana kutoacha kuzozana na del Bosque na baadaye alipanda baiskeli na kuondoka eneo la mazoezini.
CHANZO SALEH JEMBE

Post a Comment

emo-but-icon

item