KAULI YA KWANZA YA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUSHINDWA KUCHUKUA TUZO ZA MTV MAMA-2014
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kauli-ya-kwanza-ya-diamond-platnumz.html
Macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini, sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana
wetu toka nyumbani Tanzania akiwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana
kwenye tuzo hizo tena akiwa katika vipengele viwili,ingawa bahati
haikuwa njema kwa Diamond kwani hakufanikiwa kupata tuzo yoyote.
Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz
ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii:
"Maisha
ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa
MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo…
pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi
kufanya vyema….
"Shukrani
zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family,
wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo
kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next step #BET!!!… Asante
sana #Sheriangoi kwa Suti Hii".
Diamond Platnumz alikuwa pia ni mmoja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa
tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido
ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia
nyumbani kupitia DSTV.
