Kampeni ya Diwani Bonnah Kaluwa wa Kipawa ya kuchangia damu yafikia kilele
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kampeni-ya-diwani-bonnah-kaluwa-wa.html
Meya
wa Ilala, Jerry Silaa akifungua rasmi tamasha la kuchangia damu katika
viwanja vya Stakishari, Majumbasita, Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo ya
siku 10 iliratibiwa na Diwani wa Kipawa Bonnah Kaluwa (CCM).
Meya
Silaa akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama kabla ya
kuchangia damu ili kuwaokoa wagonjwa wakiwemo wakina mama wajawazito
katika viwanja vya Sitakishari Majumbasita, Dar es Salaam.
Meya
wa Ilala, Jerry Silaa akiugulia maumivu ya sindano wakati akitoa damu
ili kuwaokoa wagonjwa wanaohitaji damu katika hospitali mbalimbali
wakiwemo wajawazito bila kuwasahau madereva na abiria wa bodaboda
wanaoandamwa na ajali.
Diwani
wa Kipawa, Bonnah Kaluwa naye akidhihirisha azma yake ya kuchangia damu
kwa vitendo katika kilele cha kampeni yake ya kuchangia damu jana
katika viwanja vya Sitakishari, Majumbasita ambapo mamia ya wakazi wa
Dar es Salaam walijitokeza.
Mwakilishi
wa Chuo cha Diplomasia, Kennedy Ndosi (katikati) aliyewahamasisha
wanafunzi wa Chuo hicho waliofika kuchangia damu akiwasikiliza Meya
Silaa na Diwani Bonnah wakati wa tamasha hilo.Meya Silaa na Mganga Mkuu
wa Manispaa ya Ilala, Dk Willy Sangu (kulia) wakiondoka baada ya
kumaliza zoezi la kuchangia damu katika tamasha lililoandaliwa na Diwani
wa Kipawa, Bonnah Kaluwa katika Viwanja vya Sitakishari leo.