IMANI ZAKISHIRIKINA ZIMEKUA ZIKI GONGA MIOYO YAWENGI HUKO WILAYANI KAHAMA
Jinsi Bi Rebeka alivyopigwa shoka kichwani hadi ubongo kutoka nje
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/imani-zakishirikina-zimekua-ziki-gonga.html
Bibi
mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,
Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile
kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu
asubuhi katika Mtaa wa Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka
alienda nyumbani kwa mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na
mke wa Bundala kusaidia kuanika Dengu.
| Muonekano wa Mwili wa Marehemu kwa nje |
Imeelezwa
kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley
Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala muda huo baada ya kuitwa
na Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
