HODGSON AMUOMBA GERRARD KUICHEZEA ENGLAND FAINALI ZA ULAYA 2016
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/hodgson-amuomba-gerrard-kuichezea.html
Utabakia Stevie? Hodgson ana matumaini ya kutompoteza Gerrard.
ROY Hodgson atajaribu kumshawishi Steven Gerrard ili aendelee kucheza soka la kimataifa mpaka 2016.
Nyota huyo amebaki njia panda juu ya
hatima ya soka lake la kimataifa kutokana na matokeo mabaya ya kombe la
dunia, lakini bado anahitajika na klabu yake ya Liverpool itakayoshiriki
michuano ya UEFA msimu ujao.
Japokuwa Gerrard, 34, ameshindwa
kutamba kombe la dunia, thamani yake na uzoefu wake unahitaji katika
kikosi cha England na Hodgson anatamani kuona anaendelea kucheza licha
ya vijana wengu kuchipukia kwasasa.
Frank Lampard anajiandaa kustaafu soka
la kimataifa, kwahiyo Gerrard atabaki mchezaji pekee mkongwe na England
haitaki kumpoteza kwasababu anawaunganisha vijana katika kikosi hicho.
Marafiki au maadui?: Luis Suarez akimpa pole Gerrard baada ya kufanya vibaya kombe la dunia
Hata hivyo,
Gerrard ataifikiria klabu yake ambayo ina mechi ngumu msimu ujao baada ya kufuzu UEFA.
Gerrard amesema atafanya maamuzi baada
ya kuzungumza na marafiki, familia na kocha wa Liverpool, Brendan
Rodgers baada ya kombe la dunia.
Mawazo Rodgers yatakuwa muhimu zaidi
na inaonekana kocha wa Liverpool na madaktari wa timu watapenda kumpa
mapumziko Gerrard baada ya kombe la dunia.
Hata kama mwenyekiti wa FA , Greg
Dyke amemhakikishia kazi Hodgson mpaka 2016 licha ya kuchemsha kombe la
dunia, mechi ya mwisho dhidi ya Costa Rica itakuwa muhimu sana na kama
England itapoteza, kocha huyo atakuwa katika mazingira mabaya.
Gerrard akiwatazama wachezaji wa Uruguay walipokuwa wanashangilia bao la pili na la ushindi.