Ghana 1-2 Marekani
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ghana-1-2-marekani_16.html
02:57 Marekani imeshinda kwa mara ya kwanza katika mechi tatu za kombe la dunia dhidi ya Ghana .
02:56 Marekani imelipiza kisasi cha kushindwa katika michuano miwili ya kombe la dunia na Ghana .02:52 Ghana 1-2 Marekani
02:50 Dakika 5 za ziada .
02:49 John Anthony Brooks anaiweka Marekani 2-1 kwa kichwa
02:49 GOOOOOOOOAL
02: 48 Kona kuelekea Ghana
02:45 Andrew Ayew aisawazishia Ghana 81''
02:44 Ghana 1-1 Marekani
02:43 GOOOOOOOAL
02:35 Offside, Daniel Opare anammegea Kevin-Prince Boateng pasi safi lakini ameotea.
02:31 Mohammed Rabiu anaondoka .

Bao la pekee kufikia sasa la Dempsey dakika ya 1
02:31 Ghana imemiliki mpira asilimia 60% Marekani 40 %
02:29 Kona kuelekea lango la Ghana
02:28 Kevin-Prince Boateng atuma mkwaju juu ya lango
02:26 Marekani inazidi kuhimili wimbi baada ya wimbi ya mashambulizi ya Ghana.
02:26 Marekani 1-0 Ghana 66''
02:25 Kona kuelekea lango la Marekani
02:24 Gyan anafuma mkwaju ambao unapanguliwa na Tim Howard .
02:21 Matokeo bado ni Marekani 1-0 Ghana dakika ya 60''
02:20 Andrew Ayew anatuma mkwaju unaopaa na kwenda nje
02:19 Badiliko :Kevin Prince Boateng anachukua nafasi ya Ayew
02:17 A. Gyan apoteza nafasi nzuri ya kuiswazishia Black Stars

Ghana iliwahi kuishinda Marekani mara 2 je watawahi mara hii
02:11 Germaine Jones ahimili mashambulizi ya Ghana ndani ya eneo
02 :07 A. Gyan anapigwa mweleka nje ya eneo na ni Freekick kuelekea lango la Marekani.
02:07 Marekani 1-0 Ghana
02:07Mpira umeanza tena kipindi cha pili.
01:50 Kipindi cha kwanza kimekamilika Ghana 0- 1 Marekani
01:49 Marekani 1-0 Ghana
01:48 Sulle Muntari anakanyagwa kichwa lakini refarii anasema si hoja mechi iiendelee

Mashabiki wa Marekani washangilia bao la Dempsey
01:45 Dakika 5 za ziada ya kipindi cha kwanza
01:39 Marekani inaongoza Ghana 1-0 kunako dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza
01:39 André Ayew (Ghana) aangushwa nje ya eneo
01:23 Jozy Altidore anaondolewa uwanjani kwa machela.
01:21 Altidore ananguka chini akishika paja la kushoto
01:15 Black stars inatafuta bao la kusawazisha baada ya Dempsey kuwatamausha na bao la sekunde ya 30 ya dakika ya kwanza .
01:15 Asamoa Gyan ajiangusha mbele ya lango akiwa amesalia na kipa pekee
01:13 Offside Ghana. André Ayewautuma mpira mbele ya lango lakini , Christian Atsu anasemekana ameotea
01:06 Marekani 1-0 Ghana dakika ya 5''

Ghana inatafuta ushindi dhidi ya Marekani
01:01 Marekani inafunga bao lake la kwanza kupitia kwa Clint Dempsey chini ya sekunde 30 tangu kipenga cha kuanza kwa mechi hii.
01:00 GOOOOOOOOAL !
01:00 mpira umeanza Ghana 0-0 Marekani.

Mashabiki wa Ghana kabla ya mechi dhidi ya Marekani
00:56 Hakuna anayeweza kusahau matukio yalioikumba Black stars ya Ghana katika mchuano wa 2010 Afrika Kusini.
00:55Black stars ya Ghana inafungua kampeini yake ya Brazil 2014 dhidi ya Marekani katika uwanja wa Estadio das Dunas ulioko Natal
