FIRKA NJE YA BOKSI: BADILI CHANZO CHA TAARIFA (7)
Baada ya kutazama fikra tata na chanzo sahihi na kisicho sahihi wiki iliyopita ( bofya hapa kusoma ), leo tunaendelea na vyanzo vya mu...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/firka-nje-ya-boksi-badili-chanzo-cha.html
Baada ya kutazama fikra tata na chanzo sahihi na kisicho sahihi wiki iliyopita (bofya hapa kusoma), leo tunaendelea na vyanzo vya muono wako juu yako.
VYANZO VYA MUONO WAKO JUU YAKO
1. MAWAZO/FIKRA MGANDO:
Fikra
mgando hii si kwa watu wasiowaza sahihi tu,inawezekana na wewe unawaza
kwa namna iliyosahihi lakini fikara yako ni mgando.Fikra mgando ni ile
hali ya mtu kuridhika na kile kitu alichonacho hata kama ni sahihi.Aina
ya ulimwengu tunaoishi hata ulimwengu uliopita siku hazigandi na wala
hazitakoma kama jinsi vile sekunde zinavyotembea na kuzaa dakika dakika
nazo kwa muendelezo wake hivyo ndivyo fikra yako inavyotakiwa kufanya
kazi na kuchakata mambo.Kama jinsi vile ulimwengu unavyobadilika ndivyo
hivyo na taarifa hubadilika inaweza ikawa ni kweli kwamba jna ulifanya
jambo kwa njia hiyo na likawa ni sahihi lakini kuna uwezekano mkubwa
jambo lile lile ukajaribu kulifanya kwa njia ile ulioitumia jan na
lisilete matokeo sahihi uliyoyategemea,Hii inatufunza hapa kwamba
tunatakiwa kujiongeza katika fikra zetu tuiruhusu fikra kuwaza tene ne
tena na kuruhusu kupokea fikra sahihi na mpya kila siku ili tuondokane
na fikra mgando. kuna baadhi ya watu wakikosea jambo na ukitaka
kuwasahihisha jibu lao hua ‘MIMI/SISI NDO WA HIVI HIVI AU HIVI NDIVYO
HUA TUNAFANYA’.Unaona aina hii ya kauli inajumuisha kundi flani la watu
ambao wao wanaamini kwamba ndio wa hivyo hivyo.Ukiamini kwamba wewe ndo
wa hivyo hivyo ulivyo basi maisha yako na muono wao juu yako utakua
hivyo hivyo jinsi ulivyo na hata kama ni kweli unawaza sawa lakini
kwasababu hujaruhusu taarifa mpya iliosahihi kukufikia utaendelea kuwaza
mawazo sahihi lakini mawazo mgando au mawazo yaliopitwa na wakati. 2. KUIDANGANYA NAFSI YAKO:
Inaweza ikawa ni kauli ngumu na ngeni pia kwamba ni kwa namna gani mtu
anaweza kuidanganya nafsi yake,Nataka nikujuze tu kwamba ni mara nyingi
sana tumekua tukifanya hivyo bila hat kujua wakati mwingine.Kuna namna
ambayo unajihisi upungufu wa kitu fulani ndani ya nafsi yako au unasikia
kabisa ndani yako kuna jambo linakataa laqkini kwasababu fulani binafsi
unatoa matokeo tofauti kwa nje.Mfano rahisi ni huu....unaweza ukahisi
kabisa ndani ya nafsi yako kwamba sijisikii upendo wa kimahusiano na mtu
fulani anaweza kua ni mwanamke au mwanaume lakini kwasababu pengine za
uwezo wa kifedha au nafasi alionayo au kuna vitu unavihitaji kutoka
kwake unajikuta unalazimisha hali ya kujihisi unapenda wakati ukweki wa
ndani ya nafsi unakataa huku ndiko kuidanganya nafsi yako.Au wakati
mwingine mtu unaweza ukawa unajijua una tatizo fulani na kulingana na
lile tatizo ulilonalo kuna aina fulani ya maisha unatakiwa kuishi,lakini
unakua na ki hali fulani cha kutojali au kupotezea uhalisia wa ndani na
kuyafuata matakwa yako ya nje.Kuna baadhi ya watu mnaweza kujiuliza
lakini hii unayoisema si ni IMANI?Jibu ni rahisi sana kwamba HAPANA hii
si imani kwasababu imani haipingi ukweli uliopo lakini imani inaanza
kufanya kazi pale ukweli wa japo unapoishia,kwamba ni kweli kwamba
ninaumwa na kwa ugonjwa huu madaktari wanasema siwezi kupona na ndivyo
ilivyo sasa imani hapa inaanzia hapa...Ni kweli madaktari wamenipima na
hali yangu si nzuri lakini.... kutokana na......Ninaamini kwamba
nitapona..Kwasababu ya..!Imani mara zote ni lazima iwe na viambatanishi
na imani haipingani na ukweli lakini imani inasema kinyume na hali
halisi na kufanya yasiyowezekana kuwezekana.
JINSI YA KUBADILI MUONO WAKO WA NDANI
1. TAFUTA TAARIFA MPYA
Moja kati ya vitu vinatukwamisha sana katika maisha yetu pale
inapofikia mahali ntu unadhani umejitosheleza kwa kila kitu hasa kwenye
sehemu ya taarifa za maarifa.Kama jinsi ambavyo nilisema mwanzo kwamba
ulimwengu haujaganda hivyo pia ubongo wako hautakiwi kuganda kwa taarifa
ile ile ilioisikia jana na kutaka ikuletee matokeo mapya, ukitaka
matokeo mapya tafuta taarifa mpya.Hivi ndivyo watu waliofanikiwa kwenye
maeneno mbali mbali wanavyoishi hakuna wakati ulifika wakakaa chini na
kuridhika,kuridhika ni tabia ya umasikini tafuta maarifa mapya kila siku
tafuta changamoto mpya hiyo itakusaidia sana kubadili muono wako juu
yako
Tukutane wiki ijayo ambapo tutaendelea kutazama namna ya kubadili muono wako wa ndani..
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com