BREAKIN NEWZZ!!:- RAIS WA CHUO KIKUU CHA BUGANDO MWANZA BAADA YA UTATA WA KUPOTEA KWAKE AMEOKOTWA JANA USIKU AKIWA HANA FAHAMU HABARI LIVE!!
Bw.Mussa Leonard Mdede Aliyesimama.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/breakin-newzz-rais-wa-chuo-kikuu-cha.html
Bw.Mussa Leonard Mdede Aliyesimama. |
Rais wa chuo kikuu cha CUHAS (Bugando)
na Mwenyekiti wa Shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu nchini (TAHLISO),
Bw.Mussa Leonard Mdede ameokotwa usiku huu katika maeneo ya Usagara nje kidogo ya jiji la Mwanza, akiwa amepoteza fahamu
(hajitambui) lakini hana majeraha yoyote na amepelekwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili
ya vipimo na kupatiwa matibabu.Kwa sasa ameweza kuongea (japo kwa taabu) lakini hakumbuki chochote kilichotokea.
Bw.Mdede alitoweka ghafla siku ya
jumatano tar.18 mwezi huu, saa kumi jioni,na haikuweza kufahamika mara
moja yupo wapi, mpaka usiku huu taarifa za kupatikana kwake
zilipotolewa.
Taarifa hizi
zimedhibitishwa na Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo,
Bw.Benjamin Thomas. Taarifa zaidi juu ya hali ya Bw.Mdede zitazidi
kutolewa kwa kadri zinavyopatikana.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mwanza ameahidi kutoa taarifa leo.