Boko Haram wafanya mauaji mapya -Nigeria
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/boko-haram-wafanya-mauaji-mapya-nigeria.html
BBC imepata taarifa kuwa zaidi ya watu 20 maeuawa katika mashambulio katika vijiji vya jimbo la Borno.
Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa
juu ya hatma ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundo hilo
yapata siku 50 zilizopita.Wakaazi wa kijiji cha Attagara karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha
madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo
imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia
wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa
wakaazi wa maeneo mengi kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na
mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.