Barabara mradi mabasi mwendo kasi ni janga.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/barabara-mradi-mabasi-mwendo-kasi-ni.html
Wakati
wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa na matumaini makubwa ya
kuondokana na msongamano wa magari kutokana na ujenzi wa barabara ya
mabasi yaendayo haraka (BRT), uchunguzi umebaini kwamba mradi huo
utaleta maafa makubwa.
Imethibitika
kwamba barabara mpya inayojengwa sambamba na ya mabasi yaendayo haraka,
imepunguzwa upana wake kutoka mita sita hadi tano, hivyo kufanya
madereva kuwa na wakati mgumu wakati wa kupitana (overtake).
Upana wa mita tano kila upande ni kuanzia kwenye ukingo wa barabara ambako umejengwa ukuta (capstone).
Kuna kila
dalili kuwa mradi huu ambao umekuwa gumzo kwa kila kiongozi anayetoa
majibu ya kuondoa msongamano jijini Dar es Salaam, umegubikwa na
ufisadi.
Ufisadi
huu unatokana na ukweli kwamba wakati Mtaalamu Mwandamizi wa masuala ya
usafirishaji wa Benki ya Dunia (WB), Mhandisi Yonas Mchomvu, anasema kwa
mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa katika BRT, barabara hiyo
ingehamishiwa pembeni mwa ile ya mradi, ikiwa na upana sawa na ule wa
awali, hali ni kinyume chake.
"Labda
kama ni kwa mtazamo wa macho na baada ya kuweka zile kingo, upana wa
barabara ile ukaonekana ni mdogo, lakini ilipaswa 'kusogezwa' kwa vipimo
vya awali," anasema alipozungumzia mradi huo hivi karibuni.
Hata
hivyo, NIPASHE ilipima barabara hiyo eneo la Kimara-Korogwe na kubaini
kwamba upana wake ni mita tano upande mmoja na mita upande wa pili.
Upande
huo ni tofauti kabisa na ule ulikuwako awali wa mita sita kila upande,
huku kukiwa na upana wa mita 1.5 kila upande kwa ajili ya waendesha
baiskeli na watumiaji wengine.
Upanda
huu mdogo wa sasa mbali ya kuwa kikwazo cha kutatua foleni na
msongamano, pia unaibua suala muhumu wa thamani ya fedha katika mradi
huo unaotokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia ulitazamiwa kutumia dola
za Marekani milioni 290 (Sh. bilioni 493 (kwa viwango vya Dola moja kwa
Sh. 1,700).
NIPASHE
imethibisha kwamba katika barabara kuu nne za Dar es Salaam, Mandela,
Sam Nujoma na Ali Hassan Mwinyi zote zina upana wa mita sita na
kuendelea, huku ya Morogoro inayojengwa upya ikiwa na upana wa mita
tano.
Mandela ina upana wa mita sita kila upande, Sam Nujoma mita 6.5 kila upande na Ali Hassan Mwinyi mita sita kila upande.
Hofu ya
udanganyifu katika barabara ya Morogoro inazidi kuwa na nguvu kwani
vipimo vilivyochukuliwa na NIPASHE eneo la Kimara –Gereji ambako
haijajengwa upya umeonyesha kuwa ina upana wa mita sita na pembeni mita
1.5 kila upande, hivyo kuonyesha dhahiri kuwa eneo la kuanzia mradi BRT
Kimara –Mwisho hadi makutano na Bibi Titi Mohammed, barabara hiyo
imeminywa sana.
Kulingana
na upana huo mpya ambao ni dhahiri unaibua suala la usalama kwenye
barabara hii, kiasi cha mita mbili zilizopunguzwa, kinaibua suala
jingine ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijulikani kimekwenda wapi.
Kipande
cha barabara ya Morogoro kutoka Kimara- Mwisho hadi makutano na Bibi
Titi Mohamed, kinakadiriwa kuwa na urefu kilomita 15. Upana wa mita
mbili unaopungua katika barabara hiyo ni sawa na urefu wa barabara yenye
kilomita tano ikiwa na upana wa mita sita.
Kwa
mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Ujenzi gharama za ujenzi wa kilomita
moja ya barabara kuu ya lami inakadiriwa kufikia Sh. bilioni 1. Kwa
maana hiyo, ni dhahiri kwamba kiasi 'kilichookolewa' kwa eneo
lililopunguzwa kinafikia Sh. bilioni 5.
Hakuna taarifa zinazoeleza bayana sababu za kupunguzwa kwa upana huo wala mahali fedha 'zilizookolewa' zilipopelekwa.
Mbali na
suala la uwezekano wa ufisadi katika mradi huu, mfumo wa ujenzi wake
ambao umeongeza kona nyingi, nao umezidisha mazingira hatarishi
yanayoweza kusababisha ajali za mara kwa mara kama ilivyowahi kutokea
kwa nyakati tofauti hivi karibuni.
Siyo
Wizara ya Ujenzi wala Wakala wa Usimamizi wa Barabara Dar es Salaam
(Tanroad), walitoa maelezo juu ya sababu za kuminywa kwa barabara hiyo
kwa kiwango hicho.
Barabara ya Morogo ni mfano mmoja tu juu ya mambo yanavyokwenda ovyo katika sekta nzima ya ujenzi wa barabara nchini. uchunguzi
umebaini kuwa, ujenzi wa barabara ni miongoni mwa miradi ya maendeleo
ambayo ufujaji wa fedha za umma unafanyika kwa namna tofauti, sehemu
kubwa ikielekezwa katika huduma za kitaalamu.
Hujuma
zinazofanywa katika miradi ya barabara, zimekuwa chanzo kikuu cha ujenzi
duni unaochangia kuharibika kwa miundombinu hiyo muda mfupi baada ya
kukamilika kwake.
Kwa
kawaida, barabara zinazojengwa kwa viwango tofauti vya lami,
zinatarajiwa kutumika kwa kati ya miaka 10 hadi 16 kabla ya kufanyiwa
matengenzo makubwa.
Lakini barabara hizo zimebainika kuharibika chini ya muda huo baada ya kukamilika kwake.
UPUNGUZAJI WA VIPIMO VYA BARABARA
Moja ya mbinu zinazotumiwa na wadau wanaoshiriki ujenzi na kuikagua miradi ya barabara, ni kupunguza vipimo vya upana kwa kiasi kidogo kisichoweza kugundulika kwa urahisi hususani na wananchi wa kawaida.
Moja ya mbinu zinazotumiwa na wadau wanaoshiriki ujenzi na kuikagua miradi ya barabara, ni kupunguza vipimo vya upana kwa kiasi kidogo kisichoweza kugundulika kwa urahisi hususani na wananchi wa kawaida.
Vyanzo
tofauti vilivyofanikisha kufichuka kwa siri hiyo vinaeleza kuwa, mbinu
hiyo inatekelezwa ili kuokoa kiwango cha fedha kwa mkandarasi, ambazo
hata hivyo hazirejeshwi hazina, bali kuwafikia watu binafsi.
Hata
hivyo, taarifa zinazohusu ufisadi huo zinapatikana huku vyanzo vyake,
vikisisitiza usiri wa kutojulikana, kwa sababu za usalama binafsi na
ulinzi wa ajira zao.
HALI ILIVYO SINGIDA
Mmoja wa wahandisi katika Manispaa ya Singida, ambaye hataki jina lake litajwe gazetini, anasema kwa miaka mingi, miradi ya ujenzi wa barabara imekuwa ikihujumiwa kwa namna tofauti.
Mmoja wa wahandisi katika Manispaa ya Singida, ambaye hataki jina lake litajwe gazetini, anasema kwa miaka mingi, miradi ya ujenzi wa barabara imekuwa ikihujumiwa kwa namna tofauti.
Mhandisi
huyo, anatoa mfano wa ufisadi unaofanywa kupitia upunguzwaji wa vipimo
vya barabara, umekithiri kwenye miradi nyingi na kwamba inasababisha
upotevu wa fedha na kudidimiza ubora wa miundombinu hiyo.
Chanzo
hicho kinaeleza kuwa, kwa kawaida barabara nyingi kama zinazounganisha
mikoa, zimekuwa zikijengwa kwa upana unaofikia mita nane.
Lakini,
barabara hizo zimekuwa zikipunguzwa kwa kipimo (mathalani) cha kuanzia
mita 0.5 hadi moja na ambazo si rahisi kubainika pale ujenzi wa mradi
unapokamilika.
"Unapojenga
barabara na kupunguza mita 0.5 kutoka upana wa mita nane, si rahisi
ikagundulika kwa watumiaji wa barabara isipokuwa mpaka kwa wanaohusika
na upimaji," kinaeleza chanzo hicho.
Chanzo
hicho kinaeleza kuwa, kiasi kama hicho kinapopunguzwa, kinaokoa fedha
kwa kadri ya urefu wa barabara, ingawa kwa ujumla wake, fedha
zinazopotea ni nyingi.
"Hapa
unaweza kuziona mita 0.5 ni ndogo, lakini kwa hakika zinapojumuishwa kwa
urefu wa barabara yote, unakuta ukubwa wake unahusisha kiasi kikubwa
cha fedha kinachoishia mifuko mwa wajanja wachache," kinaeleza.
MIRADI YA WAFADHILI
Ingawa ni hivyo, imebainika kuwa miradi mingi ya barabara inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani, ama mikopo pasipo kuwapo usimamizi madhubuti, imetekelezwa kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na thamani ya fedha.
Ingawa ni hivyo, imebainika kuwa miradi mingi ya barabara inayojengwa kwa kutumia fedha za ndani, ama mikopo pasipo kuwapo usimamizi madhubuti, imetekelezwa kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na thamani ya fedha.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Juma Malik
Akil, anasema ushahidi wa kimazingira unaonyesha kutokuwapo usimamizi
mzuri wa miradi hiyo, hivyo kusababisha kiwango duni cha barabara
zinazojengwa.
"Hizi
barabara zinazojengwa na kufuatiliwa kwa karibu na wafadhili, kwa kiasi
fulani zinakuwa na ubora unaotakiwa, lakini zinazosimamiwa na mamlaka za
ndani ya nchi, hapo kuna matatizo sana," anasema alipokutana na ujumbe
wa WM mjini Unguja hivi karibuni.
Miongoni
mwa barabara zilizojengwa kwa ufadhili wa WB visiwani Zanzibar na
zinazotajwa kuwa miongoni mwa zenye ubora ni zile za Paje-Pingwe,
Matembwe-Pongwe na Mkwajuni-Nungwi.
SHINIKIZO LA MADIWANI/WABUNGE
Uchunguzi huo unabaini kuwa shinikizo za kisiasa zimekuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochochea ujenzi duni wa barabara hususani zinazounganisha maeneo ya ndani ya mikoa.
Uchunguzi huo unabaini kuwa shinikizo za kisiasa zimekuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochochea ujenzi duni wa barabara hususani zinazounganisha maeneo ya ndani ya mikoa.
Shinikizo
za kisiasa, zinatajwa kupitia vikao vya mabaraza ya madiwani, ambapo
wawakilishi wa wananchi wakiwamo wabunge ni wajumbe wake.
Mhandisi
wa jiji la Arusha, Afwilile Lamsy, anasema katika utumishi wake kwenye
fani hiyo kwa zaidi ya miaka 10, ameshuhudia kuwapo madiwani na wabunge
wanaoshinikiza ujenzi wa barabara kuyafikia maeneo wanayoamini kuwapo
wapiga kura wengi.
Mhandisi
Lamsy, anasema shinikizo hizo zinafanywa wakati ambapo bajeti za
halmashauri husika zinaposomwa na fedha kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa
barabara hasa kwa kiwango cha lami.
Inapotokea
hali hiyo, baadhi wa wabunge na wenye nguvu ya kufanya maamuzi,
wamekuwa wakihitaji mgawanyo wa fedha kidogo zinazotengwa, kuelekezwa
kwenye ujenzi ama ukarabati wa barabara nyingi na zenye urefu mkubwa,
pasipo kuwianisha na fedha zilizopo.
"Wapo
wataalamu waadilifu wanaobuni mikakati mizuri ya ujenzi wa barabara,
lakini inapowasilishwa na kujadiliwa kwenye baraza la madiwani,
wawakilishi hao wa wananchi wanaipinga," anasema.
Kwa mujibu wa Mhandisi Lamsy, hali hiyo ipo katika maeneo mengi ya halshauri za wilaya, manispaa na majini nchini.
Anatoa
mfano kuwa, inaweza kutokea wahandisi wakapendekeza kujengwa barabara
tatu kati ya 10 zilizopo kwenye halmashauri husika, kila moja kwa
kilomita moja ya kiwango cha lami.
"Lakini
ikifikishwa baraza la madiwani, wanapinga na kutaka fedha zilizotengwa
zitumike kujenga barabara nyingi ikibidi zote kwa kupitisha greda na
kumwaga vifusi," anasema.
Barabara
ni miongoni mwa miundombinu inayoligharimu taifa fedha nyingi na ambayo
kama usimamizi wake ungefanikisha kuwapo kwa ubora, ni dhahiri kwamba
zingechochea kasi ya maendeleo na kurahisisha mawasiliano.
CHANZO: NIPASHE
CHANZO: NIPASHE