BALOTELLI `CHIZI KWELI` AHITAJI BUSU LA SHAVUNI KUTOKA KWA MALKIA WA UINGEREZA KAMA ITALIA ITAIFUNGA COST RICA LEO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/balotelli-chizi-kweli-ahitaji-busu-la.html
Balotelli ametweet: 'kama tutawafunga Cost Rica, nataka busu, hasa kwenye shavu, kutoka kwa Malikia wa UK".
Nyota huyu mtukutu aliifungia bao la
ushindi Italia ikishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya England katika mchezo wa
kwanza wiki iliyopita na leo hii ataongoza mashambulizi tena mjini
Recife.
Kama vijana wa Cesare Prandelli's men watavuna pointi tatu leo, England watahitaji kumfunga Cost Rica jumanne, huku wakiombea Italia imfunge Uruguay usiku huo huo.
Wakati huo huo Prandelli anatarajia kuibeba Cost Rica leo usiku.
Balotelli anatarajia kuwa nyota wa mchezo wa leo dhidi ya Costa Rica... na ndivyo England wanataka.
Prandelli alisema Italia walijua kabla kuwa watahitaji muda kuendena na kasi ya mashindano na hali ya hewa ya Brazil.
"Tuko tayari. Sidhani kama tutakuwa na
la kujitetea," alisema. "Hali ya hewa haitishi tena. Kikosi ndio
kinatisha-kikosi kinachoongezeka kasi wakati wa mechi".
"Kwa hiyo kesho (leo), sidhani kama tutafungwa. Nina amini tutahangaika, lakini tuna mawazo ya nini tunaenda kufanya uwanjani".
Eneo la Forecasts lina mvua na joto linalokadiriwa kufikia 30C.