Flatnews

BAADA YA POLISI KUYAFANYIA "UMAFIA" MALORI YALIYOKUWA YAKIEGESHWA BARABARANI SASA YATII SHERIA, JIONEE MWENYEWE


 Malori yakiwa yameegeshwa nje ya barabara
Barabara nyeupeeeeeeee
Kufuatia askari wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam kuamua kuyafanyia "umafia" malori yanayoegeshwa barabarani eneo la tabata relini, kwa kufungua namba na kuondoka nazo, hivi sasa madereva hao wameshika adabu na kufuata sheria inavyosema

Mwandishi wa eddy blog aliyepita eneo hilo hii leo ameshuhudia malori hayo yakiwa yameegeshwa nje ya barabara na kupelekea magari yanayotumia barabara hiyo ya mandela kupita kwa raha tofauti na awali

Kutokana na askari kuwapa onyo na faini za mara kwa mara pasipo mabadiliko yeyote walilazimika kuzifungua namba za usajili za malori hayo na kuondoka nazo, jambo lililoonekana kuwa mwarobaini wa wao kutii sheria bila shuruti na kuegesha malori yao nje ya hifadhi ya barabara kama picha hizo hapo juu zinavyoonesha

Mwanzoni malori hayo yalikuwa yakiegeshwa barabarani kwa muda mrefu yakisubiri kwenda kupakia mizigo hali iliyokuwa ikisababisha ajali za mara kwa mara pamoja na usumbufu uzio wa lazima wa matumizi ya barabara hiyo

Post a Comment

emo-but-icon

item