Flatnews

AKIMBIWA NA MUME WAKE KISA UGONJWA WA SARATANI


 Josephine Domisian akiwa katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya kizazi.
INASIKITISHA! Mama mmoja  mkazi Karagwe mkoani Kagera, Josephine Domisian (34) ametelekezwa na mumewe aitwaye Dominic baada  ya kupatwa na ugonjwa wa  saratani ya kizazi miaka mitatu iliyopita.Akizungumza kwa uchungu akiwa katika hospitali ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road, jijini Dar mama huyo alisema awali mumewe alikuwa akimnyanyapaa kwa kumnyima msaada hata wa chakula, hali iliyosababisha wanakijiji wenzake kumsaidia fedha za usafiri wa kumpeleka Dar kwa ajili ya matibabu.“Nilisaidiwa kiasi cha shilingi 150,000 na kufanikiwa kufika hospitalini. Kule nilimuacha mume wangu na wanangu wanne, lakini nimepewa taarifa kwamba mume wangu amewaacha watoto, sasa wanalelewa na majirani na yeye ameoa mke mwingine.
Josephine Domisian akiwa amejipumzisha katika hospitali hiyo.
 “Kwa sasa napata msaada kutoka kwa wagonjwa  wenzangu au kutoka kwa ndugu wa wagonjwa ndiyo wananipa chakula na baadhi ya matumizi hapa hospitalini. Kule nyumbani wanangu wanaishi kama yatima, hawaendi shuleni maana hakuna mtu wa kuwapa huduma muhimu kama sare na vitu vingine.“Hapa hospitalini nimeruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali yangu kuwa nzuri kidogo, natakiwa kuja tena baada ya miezi sita lakini sina hata nauli ya kunifikisha kwetu na sijui nitapata wapi. Nawaomba Watanzania wanisaidie nauli ili nikawaone wanangu, naumia sana,” alisema mama huyo kwa huzuni.
Afisa uhusiano wa taasisi  hiyo, Nicolas Mshana amethibitisha kuruhusiwa kwa mama huyo. Yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana na Josephine kwa kutumia simu namba
0757 106143. 
-GPL

Post a Comment

emo-but-icon

item