WANANCHI WAMLALAMIKIA MBUNGE WAO KUZUIA MAENDELEO KWA MIAKA MINNE SASA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wananchi-wamlalamikia-mbunge-wao-kuzuia.html
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa madarasa
katika shule ya msingi ya Unyaghumpi katika halmashauri ya wilaya ya
Ikungi jimbo la Ikungi Mashariki wakati alipotembelea na kukagua ujenzi
wa madarasa katika shule hiyo ambayo maendeleo yake yamedumaa kwa miaka
minne sasa kutokana na hatua ya mbunge wa jimbo la Ikungi Mashariki Mh.
Tundu Lisu kuzuia wananchi katika kuchangia shughuli za maendeleo,
Wananchi wa kijiji hicho baada ya kuchoshwa na tabia za mbunge huyo
ambaye amekuwa akiwazuia katika shughuli za maendeleo yao. wameamua
kuanza tena utaratibu wa kuchangia maendeleo yao kwa hali na mali kama
inavyoonekana katika picha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akishiriki pamoja na wananchi hao katika ujenzi wa moja ya madarasa ya
shule hiyo , Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu
wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi (CCM.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-IKUNGI-SINGIDA)
Mwalimu
Juliana Joseph akifundisha wanafunzi wa elimu ya awali katika shule
hiyo huku wakiwa wamekaa chini katika jengo ambalo pia halijaezekwa kwa
miaka minne sasa baada ya shughuli za maendeleo kusimama katika jimbo
hilo
Akina mama wakishiriki shughuli za ujenzi wa madarasa katika shule hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinuana akizungumza na wananchi katika
kijiji cha Kibwi kwa mkorea wakati alipotembelea zahanati ambayo
imekamilika lakini haijaanza kutoa huduma kutokana na kutokuwepo kwa
nyumba za madaktari, mradi ambao ulisimama ukiwa kwenye msingi baada ya
wananchi kukatazwa kuchangia ujenzi huo na mbunge wao Tundu Lisu.
Huu ndiyo Msingi wa nyumba ya madaktari ambao ujenzi wake umesimama kutokana na wananchi kugoma kuchangia asilimia tano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mkiwa
Mama mjane Mayasa Mukhando na wananchi wenzake wakivuna uwele na mtama shambani kwake.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za
kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane Mayasa Mukhando katika
kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi Singida
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika shughuli za
kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane Mayasa Mukhando katika
kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi Singida
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM naye akishiriki
katika shughuli za kuvuna Mtama na Uwele katika shamba la mama mjane
Mayasa Mukhando katika kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi Singida
Wananchi
mbalimbali wakishiriki katika shughuli za maendeleo katika ujenzi wa
madarasa kwenye shule ya msingi ya kijiji cha Unyaghumpi wilayani Ikungi
baada ya kuanza tena utaratibu wa kushiriki kwtika shughuli za
maendeleo jimboni humo jimbo hilo linaongozwa na Mh. Tun
du Lisu CHADEMA. Mkuu wa wilaya ya Kishapu Ndugu Wilson Nkambaku akizungumza na kada wa Chama cha mapinduzi Bw. Hamisi Ngila.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mkiwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na watoto katika kijiji cha Mkiwa
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mkulima
wa kilimo cha umwagiliaji wa mbogamboga ambaye ni mkurugenzi wa kampuni
ya Singida Agricuture Company Limited Bw. AllyMohamed wakati akielezea
jinsi wanavyosindika mbogamboga hizo na kuzisafirisha katika nchi za
Ulaya, Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Singida Parseko Kone na kulia ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa mwa Singida Mgana Msindai.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM naye akishiriki
pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo katika kuchambua mbogamboga hizo.
Wafanyakzi wa kampuni hiyo wakiendelea na kazi
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi CCM akilima shamba kwa
trekta katika mashamba ya mbogamboga ya kampuni ya Singida Agricuture
Company Limited katika kijiji cha Mkiwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mipira maalum ya kumwagilia iliyotandazwa katika mashamba hayo.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakipulizia dawa shambani ili kuzuia maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya mimea.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Bw.
Ally Mohamed jinsi mitambo hii inavyogawanya maji ili kusambaza kwenye
mashamba.
Baadhi
ya wafanyakazi wakiwa na ndoo zilizojaa mbogamboga mara baada ya kuvuna
katika mashamba hayo tayari kwa kusindika na kusafirisha nje ya nchi
kwa mauzo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Bw.
Ally Mohamed jinsi mitambo hii inavuna maji kutoka katika visima vinne
vilivyochimbwa katika mashamba hayo na kupeleka kwenye bwawa kisha
kusambaza kwenye mashamba.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mbogamboga zilizotayari
kwa kusindikwa na kusafirishwa nje kutoka shambani.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaangalia maadhi ya wafanyakazi
waliovalia sare wakifanya kazi katika mashamba hayo.
Hili
ni Bwawa maalum lililotengenezwa katika shamba hilo ambalo linapokea
maji kutoka katika visima vinne na kisha kusambazwa katika mashamba
tayari kwa kumwagilia.
Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi