Taarifa Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/taarifa-rasmi-kwa-umma-kutoka-ikulu.html
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka jana jioni tarehe 6 Mei, 2014 kuelekea
Abuja, Nigeria kuhudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu
Afrika (World Economic Forum).
Mkutano
huo unaoanza leo tarehe 7 – 9 Mei, 14, utahudhuriwa na viongozi kutoka
Afrika na duniani kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili
njia mbalimbali zitakazolifanya Bara la Afrika kuumudu ukuaji wa
kiuchumi kwa pamoja na fursa za ajira zinajitokeza.
Katika Mkutano huo, viongozi pia watajadiliana jinsi ya kugharamia
miundo mbinu Barani Afrika, njia za kukuza biashara baina ya nchi zao na uwekezaji katika sekta ya kilimo barani.
miundo mbinu Barani Afrika, njia za kukuza biashara baina ya nchi zao na uwekezaji katika sekta ya kilimo barani.
Chini
ya kaulimbiu ya “Forging Inclusive Growth, Creating Jobs” viongozi pia
watajadili kwa pamoja namna ya kukuza uchumi na uwekezaji kwa
kushirikiana na sekta binafsi.
Wakiwa
Abuja viongozi pia watapata nafasi ya kujadili changamoto
zinazolikabili Bara la Afrika zikiwemo za ukosefu wa ajira, matishio ya
kiusalama, vikwazo vya usafiri barani, upungufu wa chakula na athari
kadhaa za mazingira.
Akiwa
mjini Abuja Rais Kikwete atakutana na viongozi kadhaa wa Afrika na
Dunia kwa ujumla ambao wapo Abuja wakiwemo Waziri Mkuu wa China Bw. Li
Keqian , Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu Bw. Gordon
Brown ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na viongozi
kadhaa wa mashirika ya kiserikali na kibinafsi.
………………Mwisho………………
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu-Dar-Es-Salaam
6 Mei, 2014
