SOMO: UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU
Askofu mkuu Zachary Kakobe.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/somo-uthibitisho-kuwa-yesu-ni-mungu.html
![]() |
| Askofu mkuu Zachary Kakobe. |
Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu Kristo ni Mungu.Ikiwa sisi ni wanafunzi wa
Biblia tusiwe kama wengine wanaosema kuwa Yesu si Mungu.Kama huna moyo
wa jiwe kama wengine waliotiwa upofu kiroho na kushindwa kuyaelewa
maandiko,Je,unaamini kuwa Yesu ni Mungu? Yesu ni Mungu na ushahidi
mwingi wa maandiko upo.
Somo hili lipo katika vipengere vinne vifuatavyo:-
KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA BIBLIA.
SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA NI MUNGU.
YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI MUNGU PAMOJA NASI.
YESU MWANA WA MUNGU.
Kipengere cha kwanza,
1.KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA MAANDIKO.Hapa tunaona maandiko
yakimtaja Yesu KriNasto waziwazi kuwa ni Mungu. Katika ( 1YOHANA. 5:20
) “Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja,naye ametupa akili
kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,nasi tumo ndani yake yeye aliye wa
kweli.,yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.Huyu ndiye MUNGU WA KWELI
NAUZIMA WA MILELE”.. Pia katika (YOHANA 20:26-29 ) “basi,baada ya siku
nane,wanafunzi wake walikuwamo ndani tena,na Tomaso pamoja nao.Akaja
Yesu na milango ilikuwa imefungwa,akasimama katikati,akasema,Amani iwe
kwenu.Kisha akamwambia Tomasolete hapa kidole chako;uitazame mikono
yangu;ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu;wala usiwe
asiyeamini;bali aaminiye.Tomaso akajibu akamwambia,BWANA WANGU NA
MUNGUWANGU..Yesu akamwambia,wewe kwa kuwa umeniona umesadiki;wa heri
wale wasioona wakasadiki”.YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13 )
Katika mstari 8 na 9 Filipo akamwambia,Bwana,utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia,Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue,Filipo?
Ikiwa tu wanafunzi wa Yesu hatupaswi kubabaishwa na watu ambao hawana Roho waMungu.Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kusema Yesu ni Mungu..Kwasababu hiyo,wanatumia akili tu.Hawa ni watu wa tabia ya asili ambao hawawezi kuyaelewa mambo ya kiroho ( 1WAKORITHO 2:14 ) “Basi,mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuyapokea mambo ya Roho wa Mungu;maana kwake ni upuuzi;wala hawezi kuyafahamu;kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni”
2.SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU.
1.YESU NI MUUMBAJI.
Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesuaitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.
2.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.
( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.( MIKA 5:2 ) “Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.
Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58). Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwaanakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ). Imasema “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega ,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 )
