Ni
katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel mjini Shinyanga ambako
kumefanyika sherehe ya uhuru wa vyombo vya habari katika mkoa wa
Shinyanga ambako waandishi wa habari zaidi ya 30 kutoka mkoani Shinyanga
pamoja na wadau wa habari mkoani humo wamejumuika pamoja katika siku
hii muhimu ambayo hufanyika Tarehe 3 mwezi Mei kila mwaka kote
duniani,lengo likiwa kuhamasisha utendaji kazi kwa vyombo vya habari
pamoja na kuhamsisha na kuimbusha serikali na jamii kwa ujumla kuhusu
umuhimu wa vyombo vya habari.
Waandishi
wa habari wakiwa katika ukumbi wa Diamond Fields Hotel wakati wa
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kauli
mbiu mwaka huu inasema “Uhuru wa habari kwa maendeleo na utawala bora”.
Waandishi
wa habari pamoja na wadau wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa
wameinamisha vichwa chini na kukaa kimya kwa muda wa dakika moja
kuwakumbuka waandishi wa habari waliotangulia mbele za haki
 |
Katibu
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kareny Masasy
akizungumza katika sherehe hizo ambapo alisema klabu hiyo ilianzishwa
mwaka 2003 na ina jumla ya waandishiwa habari 31,huku akiitaka jamii
kuendelea kushirikiana na waandishi wa habari mkoani humo katika
kufanikisha maendeleo na utawala bora.
|
 |
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) Shija Felician
akifungua sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo ambapo
waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari wamehudhuriakatika
maadhimisho hayo.
|
 |
Mshereheshaji
katika sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari
mkoa wa Shinyanga Bi Veronica Natalis ambaye ni mwandishiwa habari na
mtangazi kutoka Radio Faraja akifanya yake katika ukumbi wa Diamond
Fields Hotel mjini Shinyanga
|
 |
Sherehe
zinaendelea ambapo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga walimpongeza
mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Hussein Kashindye kwa ushirikiano
wake na vyombo vya habari |
Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri-Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari katika
mkoa wa Shinyanga alikuwa meneja wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga Said
Pamui.
 |
Mgeni
rasmi katika sherehe hizo meneja wa benki ya CRDB mkoa wa Shinyanga
Said Pamui akizungumza katika sherehe za leo ambapo aliwaasa waandishi
wa habari kujituma katika kutafuta habari pamoja na kwamba kuna baadhi
ya wadau hawatoi ushirikiano kwao kwa kuficha habari huku akiwataka
kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na jamii |
 |
Mkuu
wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Hussein Kashindye akizungumza wakati
katika sherehe hizo ambapoa pamoja na mambo mengine aliwataka waandishi
wa habari kuandika habari zinazogusa jamii nzima badala ya kuandika
habari zinazohusu mtu mmoja na kuwataka waandishi wa habari kuunga mkono
kampeni aliyoianzisha ya “Vikongwe na makazi salama”.
|
 |
Kaimu
afisa uhusiano mamlaka ya maji safi na mazingira katika manispaa ya
Shinyanga(SHUWASA)bi Amina Mabula akichangia mawili matatu katika
sherehe hizo ambapo aliwapongeza waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
kuwa mstari wa mbele kushirikiana na mamlaka hiyo |
 |
Aliyesimama
ni meneja wa Radio Kahama,Marko Mipawa akizungumza katika sherehe hizo
ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuna baadhi ya sheria zinabana
uhuru wa vyombo vya habari hivyo kukwamisha shughuli za waandishi wa
habari hasa pale wanapohitaji kutoa taarifa flani lakini sheria inazuia
mfano taarifa kutoka jeshi la polisi ambazo msemaji pekee ni kamanda wa
polisi wa mkoa husika. |
 |
Aliyesimama
na mwandishi wa habari wa ITV na radio one bwana Stephen Wang'anyi
akizungumza katika sherehe hizo,ambapo alisema moja ya changamoto
wanazokabiliana nazo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ni kukosa
ushirikiano wa karibu na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ambapo
kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amekuwa mgumu wa kutoa ushirikiano
kwa waandishi wa habari |
 |
Aliyesimama
ni meneja wa Radio Faraja bi Moshi Abdallah Ndugulile akizungumza
katika sherehe hizo ambapo aliiomba jamii kushirikiana na waandishi wa
habari |
 |
Aliyesimama
ni bwana Chibura Makorongo akichangia mawili matatu kuhusu wadau
wasioonesha ushirikiano kwa waandishi wa habari kama ilivyo hivi sasa
kwa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ambaye amekuwa mgumu kutoa
habari kwa waandishi wa habari na wakati mwingine kusema hajui kuhusu
matukio yanayoendelea katika mkoa hata kama askari polisi wake wapo
katika eneo la tukio. |
 |
Mwenyekiti
wa kamati ya maadili katika klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Shinyanga James Thomas Makwinya ambaye ni wakili na mwanasheria wa
manispaa ya Shinyanga,akitoa shukrani wakati wa kufunga sherehe hizo
ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kufanya kazi vizuri pia aliwataka
wazingatie maadili ya kazi yao.
|
 |
Picha ya pamoja waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa habari |
 |
Ilikuwa
ni furaha mwanzo mwisho-Kila mtu alikuwa na furaha yake baada ya
sherehe hizo kumalizika wengine wakadiriki kupiga picha ya pamoja kama
unavyoona pichani,wa kwanza kushoto ni bwana Stephen Wang'anyi wa Itv na
Radio One ,akifuatiwa na bi Kareny Masasy katibu wa klabu ya waandishi
wa habari mkoa wa Shinyanga,wa kwanza kushoto ni Bi Stella Ibengwe
mweka hazina wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga. |