INASIKISHA SANA: KIJANA WA MIAKA 15 AFA MAJI WAKATI AKIOGELEA BWAWANI NA WENZAKE
Vijana waliozamia na kufanikisha kuupata mwili wa Marehemu wakiwa pembeni ya mwili huo
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/inasikisha-sana-kijana-wa-miaka-15-afa.html
Vijana waliozamia na kufanikisha kuupata mwili wa Marehemu wakiwa pembeni ya mwili huo |
Mtu mmoja
Mkazi wa mtaa Shunu kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga,
aliyejulikana kwa jina la Frank Fred mwenye umri wa miaka 15, amefariki
dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye kwenye Bwawa.
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni wakati marehemu
Frank akiogelea na wenzake katika Bwawa hilo lililopo maeneo ya KTM
wilayani Kahama, ambapo alizama kusababisha kifo chake.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi ya
kuchunga mifugo, alifika katika bwawa hilo akiwa na Panga ambalo
inasemekana alitumwa na mwajiri wake kukata majini kwa ajili ya kulisha
mifugo hiyo.
Kwa
mujibu wa Wachungaji wenzake, Marehemu Frank mara kwa mara amekuwa
akiwatizama wenzake wakiogelea huku yeye akiogopa, lakini jana aliamua
kuogelea kwa lengo la kujifunza kuogelea kama wenzake.
Akizungumza Muuguzi
mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Richard Mabagala amethibisha
kupokea mwili wa marehemu leo asubuhi, na kwamba umehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Mwili wa Marehemu Frank uhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama |
Jeshi
la polisi wilaya ya kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba taratibu za Mazishi zinafanywa na Wazazi wa Marehemu ambao ni
wakazi wa Busenda kata ya Kilago wilayani humo.