SHANGWE LA UBINGWA MAN CITY USIPIME, MAELFU YA MASHABIKI WAFUNIKA ETIHAD, PELLEGRINI ABEBWA JUU JUU!
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/shangwe-la-ubingwa-man-city-usipime.html
Mzee juu juu: Wachezaji wa Man City wakimbeba na kumrusha hewani Manuel Pellegrini
Shangwe tupu Etihad, ubingwa raha sana
KLABU ya Manchester City imebeba taji la ligi kuu nchini England kwa mara ya pili katika misimu mitatu na mchana wa leo watafanya sherehe kubwa katika dimba lao la Etihad kushangilia mafanikio hayo.
Magoli ya Samir Nasri na Vincent Kompany yaliisaidia Man City kushinda mabao 2-0 dhidi ya West Ham na kufanya ushindi wa mabao 2-1 waliopata Liverpool kwenye uwanja wa Anfield dhidi ya Newcastle usiwe na maana yoyote.
Baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, maelfu ya mashabiki wa Man City waliingia uwanjani kuwapongeza mashujaa wao.
Tazama picha hapo chini jinsi Man City walivyoshangilia kubeba ubingwa wa EPL.

