PETR CECH KUKAA NJE YA UWANJA KWA WIKI 8-10 BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI WA BEGA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/petr-cech-kukaa-nje-ya-uwanja-kwa-wiki.html
CHELSEA
imethibitisha kuwa mlinda mlango wake namba moja, Petr Cech tayari
amefanyiwa upasuaji wa bega lake na sasa anatarajia kurudi uwanjani
baada ya wiki 8 au 10.
Kipa
huyo raia wa Jamhuri ya Czech aliteguka bega lake katika mchezo wa
kwanza wa UEFA dhidi ya Atletico Madrid kwenye uwanja wa Vicente
Calderon na baada ya hapo kocha Jose Mourinho amelazimika kumtumia Mark
Schwarzer katika mechi za mwisho za msimu huu.
Hata
hivyo, mashabiki wa Chelsea wamepata ahueni baada ya klabu kuthibitisha
kuwa kipa huyo amefanikiwa kufanyiwa upasuahi na ataendelea kuimarika
wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
Taarifa
iliyoandikwa katika mtandao rasmi wa Twita wa Chelsea amesomeka: “Petr
Cech amefanikiwa kufanyiwa upasuaji leo (jana) kufuatia kuteguka beki
lake. Atakaa nje kwa miezi 8 hadi 10.”
Bado
Cech ataendelea kuwa kipa namba moja wa Chelsea msimu ujao, huku
Thibaut Courtois akitarajia kurudi katika klabu yake ya Atletico
Madrid baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo.
Cech
amecheza mechi 46 za mashindano yote msimu huu na amekuwa kipa namba
moja tangu alipojiunga na Chelsea kutoka Rennes ya Ufaransa mwaka 2004.
