Linex aligoma kuhama nchi kisa Bongofleva, sasa Mfinland anataka kurudi !
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/linex-aligoma-kuhama-nchi-kisa.html
Linex ambae ni staa wa single mpya ya ‘Onga onga’ aliwahi kutangaza kupitia AMPLIFAYA ya CloudsFM pamoja na millardayo.com kwamba ameachana na mpenzi wake raia
wa Finland ambae walikutana kwa mara ya kwanza kwenye ndege na baada ya ukarimu wa Linex mrembo akadata.
Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi mpaka Linex akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba lakini safari ikafikia mwisho miezi michache baadae baada ya mrembo huyo kurudi Finland na kumtaka Linex amfate huko wakaishi pamoja.
Linex alikata kuhamia Finland kwa kudai ameteseka kwa miaka kutafuta njia ya kutoka kimuziki Tanzania hivyo baada ya kufanikiwa hawezi kuihama nchi na kwenda kuanza maisha mapya kwa mara ya kwanza nje ya nchi wakati anategemea maisha yake yaendeshwe na muziki.
Baada ya miezi kupita ya uhusiano wao kukatika, mrembo amerudi tena kwa Linex na kumuuliza kama ni sahihi akiendelea kuvaa pete ya uchumba aliyomvalisha?
Linex anasema ‘haya ni maisha na unaweza kuona umesonga mbele lakini inafikia time kuona ulikosea hivyo unataka kurudi nyuma na ni wachache sana huwa wanafanikiwa kurudisha siku nyuma, mi sikumchunia nilikua nachat nae na kuwasiliana wakati wote ila juzi kanipigia simu ananiomba
kwa kuuliza bado anaweza kuendelea kuvaa ile pete ya uchumba?’
‘Nilimvisha
pete ya uchumba na akawa ndio Mwanamke wa kwanza kumvisha na ikawa ishu
kubwa baada ya wazazi wangu kufahamu wakakasirika kwa sababu
sikuwashirikisha…. so mrembo ananiuliza anaweza kuivaa ile pete kwa
misingi ile niliyokua naitaka wakati namvalisha? bado sijapata maamuzi
so nilimwambia hiyo haiwezi kuwa rahisi hivyo’
‘Amekua akiniuliza kama nimepata mpenzi mwingine na jibu langu ni hapana sijapata ambapo baada ya kuona nimekua mzito kutoa jibu kuhusu uvaaji wa pete hiyo ameamua kuja Tanzania mwisho wa May 2014 ili tuongee, sijui nitaongea nini kwa huyu mwanamke ambaye kiukweli ni wa tofauti kukutana nae maishani mwangu, nikimuelewa nitarudiana nae
tu kwani watu wangapi wamerudishaga majeshi kwa wapenzi wao wa siku nyingi?’
Pamoja na kuyasema hayo, Linex amesema bado anaudai huu muziki wa bongofleva na ili aweze kupata hela ni lazima afanye kazi sana na msimamo wake wa kutohama Tanzania uko palepale… ‘siwezi kuuacha huu muziki ulionifanya nitembee juu ya treni sina nauli natoka Kigoma naufata Dar, huwezi kuningo’a Tanzania hivihivi yani… Ulaya siku hizi ni pakwenda kutembea na kurudi tu’
Unadhani msimamo wa Linex ni sahihi? ungempa tena nafasi mpenzi wako baada ya kukuacha kwa miezi?
wa Finland ambae walikutana kwa mara ya kwanza kwenye ndege na baada ya ukarimu wa Linex mrembo akadata.
Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi mpaka Linex akafikia hatua ya kumvisha pete ya uchumba lakini safari ikafikia mwisho miezi michache baadae baada ya mrembo huyo kurudi Finland na kumtaka Linex amfate huko wakaishi pamoja.
Linex alikata kuhamia Finland kwa kudai ameteseka kwa miaka kutafuta njia ya kutoka kimuziki Tanzania hivyo baada ya kufanikiwa hawezi kuihama nchi na kwenda kuanza maisha mapya kwa mara ya kwanza nje ya nchi wakati anategemea maisha yake yaendeshwe na muziki.
Baada ya miezi kupita ya uhusiano wao kukatika, mrembo amerudi tena kwa Linex na kumuuliza kama ni sahihi akiendelea kuvaa pete ya uchumba aliyomvalisha?
Linex anasema ‘haya ni maisha na unaweza kuona umesonga mbele lakini inafikia time kuona ulikosea hivyo unataka kurudi nyuma na ni wachache sana huwa wanafanikiwa kurudisha siku nyuma, mi sikumchunia nilikua nachat nae na kuwasiliana wakati wote ila juzi kanipigia simu ananiomba
kwa kuuliza bado anaweza kuendelea kuvaa ile pete ya uchumba?’
‘Nilimvisha
pete ya uchumba na akawa ndio Mwanamke wa kwanza kumvisha na ikawa ishu
kubwa baada ya wazazi wangu kufahamu wakakasirika kwa sababu
sikuwashirikisha…. so mrembo ananiuliza anaweza kuivaa ile pete kwa
misingi ile niliyokua naitaka wakati namvalisha? bado sijapata maamuzi
so nilimwambia hiyo haiwezi kuwa rahisi hivyo’‘Amekua akiniuliza kama nimepata mpenzi mwingine na jibu langu ni hapana sijapata ambapo baada ya kuona nimekua mzito kutoa jibu kuhusu uvaaji wa pete hiyo ameamua kuja Tanzania mwisho wa May 2014 ili tuongee, sijui nitaongea nini kwa huyu mwanamke ambaye kiukweli ni wa tofauti kukutana nae maishani mwangu, nikimuelewa nitarudiana nae