Flatnews

HATIMAYE WILAYA YA KILOLO YAMILIKISHA MTO KWA MWEKEZAJI


VITUUGUU_94583.jpg

Shamba la vitunguu
VITUUGUU.3_73421.jpg
Msimamizi wa shamba la vitunguu la mwekezaji, Onesmo Kihaga ambaye pia ni mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kisichotumia mashine akionyesha bomba linalosafisha maji kutoka bwawani kwenda shambani.

CHEMCHEM_6db81.jpg
Chanzo cha maji kabla yakuchepushwa.
BWAWA.jpgT_235f2.jpg
Bwawa la maji
Na Matias Kanali
Wananchi wa Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Ilole wilayani KILOLO mkoani Iringa wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kwa kubinafsisha mto wa maji na kusababisha umasikini kwa wananchi wa kijiji hicho. (FS)
Read more...

City wamuudhi Toure

Published in Michezo
140427170326_yaya_toure_manchester_city_crystal_palace_512x288_getty_nocredit_178a3.jpg
140520143709_yaya_toure_ameudhika_man_city__512x288_bbc_nocredit_3cf66.jpg

Wakala wa kiungo wa Machester City Yaya Toure amekashifu kupuuzwa kwa kiungo huyo kutoka Ivory Coast.
Dimitri Seluk alikashifu ujumbe wa kheri njema kwa Toure ambaye alikuwa anaadhimisha siku kuu ya kutimiza miaka 31 mnamo mei tarehe 13.
Ujumbe huo ulioambatana na keki haukumridhisha hata kidogo Seluk ambaye anasema kuwa alitarajia wamiliki wa klabu hicho angalau kumtambua kiungo huyo wa Ivory Coast ,timu hiyo ilipotua Abu Dhabi kusheherekea ushindi wao wa taji la Uingereza kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Seluk alisema Toure huenda akaondoka iwapo wamiliki wa klabu hiyo wataendelea kumpuuza.
Toure aliandikisha kandarasi mpya ya miaka minne mwaka uliopita licha ya Seluk ambaye amemuakilisha Toure kwa zaidi ya miaka kumi kutishia kuwa kiungo huyo wa Ivory Coast angehama Etihad.
Uhusiano baina ya mchezaji huyo bora barani Afrika na Seluk umedumu kwa miaka mingi kiasi ya kuwa Toure alimpa mwanawe wa pili jina la Seluk.CHANZO BBC,(A.I)
130530145842_nigeria_map_3293c.gif


Watu 17 wameuawa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya kijiji kimoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Mji wa Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu na mji wa Chibok ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria wakati nchi hiyo ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana miambili waliotekwa nyara na Boko Haram.
Juhudi hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel, Marekani na Uingereza.
Pia limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos, lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.CHANZO BBC,(A.I)

Mbu waanza kuvamia Uingereza

Published in Majuu
140330161401_mosquitoes_512x288_bbc_nocredit_2a8af.jpg
Mbu hawa wananofiwa kuanza kusababisha Malaria
140307040702_malaria_304x171_sciencephotolibrary_55341.jpg
Viini vinavyosababisha Malaria
Utafiti uliofanywa nchini Uingereza unaonyesha kuwa Mbu wameanza kuvamia maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Mabadiliko katika hewa ya mjini nchini Uingereza yameanza kutoa mazingira mazuri kwa Mbbu kuishi, ikiwemo wale wenye uwezo wa kuambukiza ugonjwa wa Malaria na virusi vijulikanavyo kama 'West Nile virus'.
Utafiti unasema kuwa mazingira ya joto pamoja na vidimbwi vya maji katika nyumba za watu, yanawaleta Mbu karibu na watu.
Mbu wanaopatikana nchini Uingereza hawana uwezo wa kuambukiza maradhi yoyote, lakini wanasayansi hao wanasema kuwa jambo la wadudu hao kuzaana katika maeneo ya mjini linaongeza uwezo wa magonjwa kulipuka.
Wanasayansi hao hata hivyo wanakusanya data zaidi kuona ikiwa wengi wa wadudu pamoja na aina ya wadudu wenyewe inaweza kuchangia kwa vyovyote mlipuko wa maradhi au la, hasa katika maeneo ya mjini.
Kadhalika wanasayansi hao wanasema kuwa kutokana na ongezeko la viwango vya joto katika maeneo ya mjini,Mbu katika baadhi ya maeneo kama vile Kusini mwa Ulaya wameweza kusababisha magonjwa.
Pia wanasisitiza kwamba Magonjwa yamelipuka katika baadhi ya mataifa ya Ulaya kutokana na mabadiliko ya tabia ya Mbu.
Zaidi ya aina 30 ya Mmbu wamepatikana nchini Uingereza
"katika maeneo ya vijijini kuna Mmbu wengi zaidi kwa sababu ya mazingira tofauti tofauti, wengine wanapenda kuishi katika nyasi , wengine katika vidimbwi, na wengine katika mashimo,'' alisema mmoja wa wataalamu.
"lakini ukienda katika maeneo ya mijini , hakuna Mmbu wengi sana , labda utapa aina mbili au tatu ya Mmbu.
Daktari mmoja kwa jina Callaghan, alisema kuwa kulikuwa na visa vingi vya ugonjwa wa Malaria kila mwaka nchini Uingereza , wengi wanaokuwa wanarejea kutoka sehemu mbali mbali za dunia ambako ugonjwa Malaria unapatikana.CHANZO BBC,(A.I)

Uchumi wa Ethiopia unaimarika kwa kasi

Published in Uchumi
131027133116_ethiopia_304x171__nocredit_e11f6.jpg
Dola bilioni nne za kimarekani kwa miundo msingi Ethiopia
131027133822_ethiopia_512x288__nocredit_414f8.jpg
Ethiopia inajitahidi kuimarisha miundo mbinu
140404081241_ethiopias_economy_304x171__nocredit_7686b.jpg
Changamoto hazikosekani katika kukuwa kwa uchumi huo

Miaka thelathini baada ya Ethiopia kukabiliwa na njaa iliyowauwa raia wengi, nchi hio ambayo ilitambulika kwa umaskini wa kukithiri sasa imeimarika na kuwa moja wapo ya nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika.
Ethiopia sasa imeanzisha mradi wa maendeleo wa kuboresha miundo mbinu ili kuinua maisha ya watu millioni 90 wa nchi hiyo.
Uchumi wa Ethiopia umeimarika katika kipindi cha miaka saba iliyopita huku shirika la fedha duniani, IMF likisema viwango vya ukuaji vimeongezeka kwa asilimia saba kila mwaka.
Na ni katika sekta ya ujenzi ambapo ukuaji huo umeshuhudiwa zaidi.
Maendeleo nchini
Ujenzi wa majumba makubwa, maeneo ya burudani na nyumba za wapangaji umeongezeka pakubwa.
Aidha ujenzi wa miundo msingi pia umetiliwa maanani.
Mwaka huu pekee, serikali ya Ethiopia imetenga takriban dola bilioni nne za kimarekani kwa ajili ya ujenzi huo.
Waziri wa fedha nchini humo, Sufian Ahmed anasema serikali itaendelea kuwekeza katika barabara na reli.
Tayari ujenzi wa reli katika mji mkuu wa Addis Ababa, umeanza na unatarajiwa kukamilishwa mwaka ujao.
Mradi huo utagharimu takribani dola milioni mia tano.
Changamoto
Licha ya hatua hizo, viwango vya umaskini ni vikubwa Ethiopia na serikali imeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa katika kupambana na mfumuko wa bei za bidha muhimu.
Ni suala ambalo waziri Ahmed anasema serikali inalitilia maanani.
Licha ya Ethiopia kukabiliwa na changamoto hizo, inasema imo katika mkondo wa kuwa taifa lenye utajiri wa kadri kufikia mwaka wa 2025.BBC,(A.I)
131219101534_mubarak_304x171_ap_nocredit_d5c5e.jpg

Hosni Mubarak wakati kesi yake ilipokuwa inaendelea


Rais aliyeondolewa madarakani nchini Misri, Hosni Mubarak amehukumiwa jela miaka mitatu.
Wanawe wawili Alaa na Gamal wamepata kifungo cha miaka minne kila mmoja.
Wendesha mashitaka walisema kuwa wanawe Mubarak waliponda mamilioni ya dola pesa za umma zilizotengewa kukarabati ikulu ya Rais na badala yake wakafanyia ukarabati nyumba zao za kifahari.
Wametakiwa kulipa pesa hizo za serikali na kutozwa faini ya dola milioni tatu.CHANZO BBC,(A.I)

"MADENI YA WALIMU KULIPWA KABLA YA JULAI"

Published in Jamii
bunge-dom_467c7.png
SERIKALI imesisisitiza kuwa italipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya walimu kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha, 2013/14. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa, alieleza hayo bungeni juzi jioni wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Bunge lilipitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/15 ya Sh bilioni 799 zikiwamo Sh bilioni 344.2 za matumizi ya kawaida na Sh bilioni 454.8 kwa ajili ya maendeleo.(Martha Magessa)
Read more...

MAPINDUZI MAKUBWA YA VIWANDA

Published in Jamii

WIZARA ya Viwanda na Biashara imewasilisha bungeni bajeti yake inayoonesha mapinduzi makubwa katika viwanda, ikiwamo kuanza kwa miradi ya chuma ya Liganga na Mchuchuma na kiwanda cha kuua viluwiluwi vya mbu waenezao malaria.
Pia kiwanda cha matairi cha General Tyre kinatarajiwa kuanza tena uzalishaji katika mwaka ujao wa fedha. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda aliwasilisha bajeti yake hiyo bungeni jana.(Martha Magessa)
Read more...

UKAWA WAMPONZA ASKOFU KAKOBE

Published in Jamii
UkawaWalivyosusa_5f2a2.png
USHIRIKA wa wachungaji wa Kipentekoste nchini (PPFT) umemtaka Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Askofu Zakaria Kakobe, kuacha tabia ya kutumia mwavuli wa dini kuhubiri chuki na uchochezi kwa wananchi.
Akizungumza juzi wakati wa kufunga semina ya viongozi wa dini wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Umoja Hostel, Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji nchini, Askofu Ikongo alisema kauli za Askofu Kakobe zimekuwa za hatari na zinaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko ya kidini.
"Nchi yetu imekuwa na dalili za viashiria vya kutoweka kwa amani na utulivu, kutokana na baadhi ya viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa na kuanza kutoa kauli za kuashiria uchochezi na kupandikiza chuki kwa waumini…sasa umefika wakati sisi viongozi wa dini hatuwezi kunyamaza kwani tutaonekana na matamko yanayotolewa kiholela kwa kutumia mwamvuli wa upentekoste," alisema Askofu Ikongo.
Alisema Askofu Kakobe amekiuka uadilifu wake, kwani Aprili 20 mwaka huu katika kanisa lake la Mwenge, alitoa kauli kuwa atapambana hadi Tanganyika irudi hata kwa kukatwa kichwa, kauli ambayo inadhihirisha ugaidi.
Askofu Ikongo alisema kauli kama hiyo haistahili kutolewa na mtumishi yeyote wa Mungu, kwani mtu mwenye uwezo wa kusema hata akatwe kichwa sio wa kawaida bali ni mtu aliye na mafunzo ya kujitoa mhanga kama gaidi.
"Tunasikitishwa na kauli za Askofu Kakobe ambazo zinaweza kuliletea Taifa machafuko ya kidini…siku ya Pasaka Aprili 20 mwaka huu aligeuza mimbari kuwa jukwaa la siasa, kwa kuhubiri uchochezi kwa kudai; kila mtu anayepigania kurudi kwa Tanganyika, ana Mungu ndani yake,” alisema.
Kwa mujibu wa Askofu Ikongo, kauli hizo za Kakobe ni za kigaidi na zina nia ya kuvuruga amani ya Watanzania na kuliingiza taifa kwenye machafuko, ambayo yataharibu tunu iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema ni vyema viongozi wa dini wajikumbushe wajibu wao wa kuliombea Taifa, na kuwaongoza waumini wao kufuata yaliyo mema badala ya kugeuka sehemu ya kutumiwa na wanasiasa.(Martha Magessa)
Read more...

Mabalozi 12 EU wamlima Pinda barua kuhusu albino

Published in Jamii

Dar es Salaam. Mabalozi 12 wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini wamemtumia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda barua ya wazi wakimtaka kuchukua hatua stahiki kwa watu waliofanya mauaji ya albino wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.
“Tumesikitishwa na mauaji ya kikatili ya albino Munghu Lugata yaliyotokea Mei 12, 2014 wilayani Bariadi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na mabalozi 12 wa nchi wanachama wa EU Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo nchini, Filiberto Sebregondi. (J M)
Read more...
IMG_8522
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akimsikiliza kwa makini  Meneja Mkuu wa KLM kwa upande   wa Africa Mashariki Bw. Dries Klein   wakati  hafla ya maadhimisho ya kutimiza  miaka 45 ya Shirika  la KLM kufanya kazi  nchini  yaliyofanyika jana jijijni Dar es Salaam.
IMG_8535
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akipongezana kwa furaha na  baadhi ya Wadau na   watendaji wa Shirika la Ndege KLM  wakati wa  hafla ya maadhimisho  maadhimisho ya kutimiza  miaka 45 ya Shirika  la KLM kufanya kazi  nchini  yaliyofanyika jana jijijni Dar es Salaam.
IMG_8586
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Lazaro Nyalandu  akipokea zawadi ya  mfano wa picha ya  Ndege ya Shirika  la  KLM katika  kilele cha madhimisho ya miaka 45 ya Shirika la KLM  kufanya kazi  nchini  yaliyofanyika jana jijijni Dar es Salaam (J M)
Canzo Fullshangwe

‘BADO SACCOS HAZIJAWASAIDIA WAJASIRIAMALI’

Published in Jamii

Waziri wa Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza.PICHA|MAKTABA 
Dar es Salaam. Ongezeko la idadi ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos), limedaiwa kutokuwa na msaada mkubwa kwa wajasiriamali wadogo.
Kauli hiyo imekuja huku serikali kupitia Waziri wa Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza ikisema vyama hivyo vimeongezeka kutoka 5,424 Machi 2012 hadi 5,559 Machi 2013. (J M)
Read more...

WAKAZI DAR WAUNGANA KUFANYA USAFI MTO MLALAKUWA

Published in Jamii


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) kukagua  mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Chanzo full shwangwe. (J M)


Arusha. Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika  katika eneo hilo. (J M)
Read more...

Meli ya Kikwete kukamilika 2016

Published in Jamii

Mwanza. Siku kama ya leo mwaka 1996, ilikuwa ni vilio kila kona ya nchi, lakini Kanda ya Ziwa iliathirika zaidi na kuzama kwa meli ya Mv Bukoba na kuteketeza mamia ya wananchi. (J M)
Read more...

Tafuta Habari

Nafasi za Kazi & Masomo

Prev Next

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJI…

  Jumla ya Walimu wapya 36,021 a...
Soma zaidi

Nafasi za kazi - Web Developers

We are looking for a talented web deve...
Soma zaidi

Nafasi za kazi - Dudumizi

We are looking for a talented web deve...
Soma zaidi

Makamanda Na Football Propaganda!

Leo wametinga mitaa ya kati Iringa Mji...
Soma zaidi

Video Gallery

Kwa video za matukio mbalimbali yanoyotokea Tanzania.

Post a Comment

emo-but-icon

item